WHO yatoa indhari: Hali ya kiafya ya Yemen ni mbaya sana
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i22597-who_yatoa_indhari_hali_ya_kiafya_ya_yemen_ni_mbaya_sana
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kuwa hali ya kiafya nchini Yemen ni mbaya sana na kubainisha kuwa tangu vilipoanza vita vya Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo hadi mwezi Novemba mwaka jana, zaidi ya watu 7,300 wameuawa na wengine ya 39,000 wamejeruhiwa.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Jan 01, 2017 13:05 UTC
  • WHO yatoa indhari: Hali ya kiafya ya Yemen ni mbaya sana

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kuwa hali ya kiafya nchini Yemen ni mbaya sana na kubainisha kuwa tangu vilipoanza vita vya Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo hadi mwezi Novemba mwaka jana, zaidi ya watu 7,300 wameuawa na wengine ya 39,000 wamejeruhiwa.

WHO imeongeza kuwa tangu vilipoanza vita hivyo, vituo 274 vya afya vimeharibiwa au kubomolewa kikamilifu.

Mbali na kuashiria kwamba vituo vya afya nchini Yemen vinakabiliwa na uhaba mkubwa mno wa dawa na kulazimika kuendesha shughuli zake bila ya msaada wowote, Shirika la Afya Duniani limetahadharisha kuwa endapo vita vitaendelea, hali hiyo itakuwa mbaya zaidi.

Lisheduni ni matokeo ya hali mbaya ya kiafya iliyosababishwa na vita Yemen 

Itakumbukwa kuwa mwezi Machi mwaka 2015, kwa uungaji mkono wa Marekani, Saudi Arabia ilianzisha mashambulio dhidi ya maeneo mbalimbali ya Yemen. Moja kati ya malengo makuu ya mashambulio hayo ya kivamizi ya utawala wa Aal Saud ni kutaka kumrejesha madarakani kibaraka wake, rais aliyejiuzulu na kuitoroka nchi Abdrabbuh Mansur Hadi. Mbali kuua na kujeruhi maelfu ya raia, mashambulio ya Saudia yameteketeza pia miundombinu ya Yemen na kusababisha mamilioni ya Wayemeni kubaki bila makaazi na kuwa wakimbizi…/