Wazayuni waongeza njama za kuuvamia Msikiti wa al Aqsa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i24571-wazayuni_waongeza_njama_za_kuuvamia_msikiti_wa_al_aqsa
Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel Knesset limefuta marufuku iliyokuwa inawazuia wabunge wa utawala huo kuingia ndani ya msikiti wa al Aqsa, ambacho ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 01, 2017 23:21 UTC
  • Wazayuni waongeza njama za kuuvamia Msikiti wa al Aqsa

Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel Knesset limefuta marufuku iliyokuwa inawazuia wabunge wa utawala huo kuingia ndani ya msikiti wa al Aqsa, ambacho ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

Kanali ya Pili ya televisheni ya utawala wa Kizayuni ilitangaza jana (Jumatano) kuwa, bunge la utawala huo limebatilisha amri ya mwaka 2015 ya kuwapiga marufuku wabunge wa Israel kuingia ndani ya msikiti wa al Aqsa. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kamati ya maadili ya bunge la utawala wa Kizayuni limewaruhusu wabunge wake kuingia msikitini humo, wakiwa pamoja na polisi wa utawala huo dhalimu.

Sheria ya kuwapiga marufuku wabunge wa Kizayuni kuingia katika msikiti wa al Aqsa ilipasishwa mwaka 2015 na iliongezewa muda mwezi Aprili 2016 baada ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni kuwashambulia Waislamu waliokuwa wanasali msikitini humo.

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakikivamia Kibla cha Kwanza cha Waislamu

 

Mashambulizi na uvamizi wa mara kwa mara wa walowezi wa Kizayuni dhidi ya msikiti wa al Aqsa ndio ambao mara zote umekuwa ukizusha mapigano baina ya Waislamu wa Palestina na wanajeshi katili wa Israel.

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limeutangaza Msikiti wa al Aqsa kuwa ni sehemu ya turathi za Kiislamu. Hata hivyo msikiti huo muhimu sana umekuwa ukivamiwa karibu kila siku na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Ikumbukwe kuwa, kadhia ya Palestina na Msikiti wa al Aqsa ndilo suala muhimu zaidi la Waislamu hivi sasa na kwamba Waislamu wa kona zote za dunia wana wajibu wa kusimama imara kukilinda Kibla chao cha Kwanza na kukimboa kutoka katika makucha ya Wazayuni.