Israel yafanya hujuma mpya za anga Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i25742-israel_yafanya_hujuma_mpya_za_anga_ukanda_wa_gaza
Jeshi la utawala katili wa Israel limefanya mashambulizi mapya ya anga katika Ukanda wa Gaza na kujeruhi watu kadhaa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 28, 2017 04:22 UTC
  • Israel yafanya hujuma mpya za anga Ukanda wa Gaza

Jeshi la utawala katili wa Israel limefanya mashambulizi mapya ya anga katika Ukanda wa Gaza na kujeruhi watu kadhaa.

Ashraf al-Qidra, Msemaji wa Wizara ya Afya ya Gaza amesema watu wanne walijeruhiwa katika hujuma hiyo ya ndege za kijeshi za Israel, katika eneo la Nahda, karibu na Rafah jana Jumatatu.

Kadhalika ndege hizo za kivita za Israel zilishambulia kwa makombora, kituo cha Harakati ya Muqawama ya Palestina Hamas, kinachojulikana kama  Shuhadaa, karibu na kambi ya wakimbizi ya Nuseirat.

Watoto wamekuwa wahanga wakuu wa hujuma za Israe, Gaza

Siku chache zilizopita, Wapalestina wawili waliuawa shahidi huku wengine zaidi ya watano wakijeruhiwa baada ya ndege ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kutekeleza hujuma ya anga katika mji wa Rafah, Ukanda wa Gaza, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Ukanda wa Gaza umekuwa katika mzingiro wa kibaguzi na kidhalimu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, tokea mwaka 2007.