Utawala wa Kizayuni na wimbi jipya la migomo
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i27494-utawala_wa_kizayuni_na_wimbi_jipya_la_migomo
Katika siku za hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshuhudia wimbi jipya la migomo. Mgomo wa karibuni kabisa ni ule wa wanadiplomasia wa ofisi za kibalozi za utawala huo dhalimu ambao wameamua kufanya mgomo wa wote kulalamikia mishahara na marupurupu madogo wanayopatiwa.
(last modified 2026-05-13T18:57:29+00:00 )
Apr 09, 2017 01:58 UTC
  • Utawala wa Kizayuni na wimbi jipya la migomo

Katika siku za hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshuhudia wimbi jipya la migomo. Mgomo wa karibuni kabisa ni ule wa wanadiplomasia wa ofisi za kibalozi za utawala huo dhalimu ambao wameamua kufanya mgomo wa wote kulalamikia mishahara na marupurupu madogo wanayopatiwa.

Maafisa 1200 wa ofisi za kibalozi za utawala wa Kizayuni walianzisha mgomo wa wote siku ya Jumatano. Wanadiplomasia hao wanalalamikia kutoongezewa mishahara yao katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, licha ya kwamba tangu hapo awali mishahara yao ni midogo.

Mgomo huo umepelekea kufungwa shughuli za ofisi nyingi za kibalozi za utawala wa Kizayuni. Wimbi jipya la migomo limeukumba utawala huo ghasibu katika hali ambayo Israel imezidi kutengwa kimataifa katika miezi ya hivi karibuni kutokana na walimwengu kukasirishwa na siasa zisizo na ubinadamu za utawala pandikizi wa Kizayuni. Mgomo wa maafisa wa kibalozi wa Israel umekwamisha pia kazi za Wizara ya Mambo ya Nje ya utawala huo.

Maandamano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel

 

Kushtadi mzozo ndani ya chombo cha kidiplomasia cha Israel kulikopelekea kufungwa shughuli nyingi za utawala wa Kizayuni kwa upande mmoja, na kuweko mivutano mikubwa baina ya wanadiplomasia na taasisi za kiusalama kwa upande wa pili ni mambo yaliyoufanya utawala ghasibu wa Kizayuni kukumbwa na msukosuko mkubwa, si upande wa kiuchumi tu, lakini pia katika upande wa kisiasa na kiusalama.

Kuzidi kuwa mbaya hali ya kiuchumi ya utawala wa Kizayuni ni matunda ya uongozi mbaya na ufisadi mkubwa wa viongozi wa utawala huo dhalimu hususan kutokana na viongozi hao kutenga bajeti kubwa katika masuala ya vita na uvamizi na kusahau kushughulikia maisha ya wakazi wake. Wimbi jipya la migomo katika idara za serikali na vituo vya kiuchumi na kibiashara inaendelea kuuburuza utawala wa Kizayuni upande wa kulemaa kikamilifu. La kukumbukwa ni kuwa, katika miaka ya hivi karibuni na hususan tangu baada ya kuundwa Baraza jipya la Mawaziri la serikali yenye misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu, Israel imeshindwa kuwa na Waziri wa Mambo ya Nje.

Hayo yanajiri katika hali ambayo wakazi wa utawala wa Kizayuni wanazidi kufanya migomo na kupinga siasa za viongozi wa utawala huo na hivyo kuifanya Israel izidi kung'ang'aniwa na kinamasi ya migogoro ya ndani. Ukweli ni kwamba migogoro inayouandama utawala wa Kizayuni si tu haina mwisho, lakini pia wigo wa migogoro hiyo unazidi kupanuka, sekunde baada ya sekunde.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel

 

Kuendelea migomo na malalamiko ya wakazi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya siasa za viongozi wa utawala huo kunaashiria kwamba, wakazi wa Israel hawana imani kabisa na Baraza la Mawaziri la hivi sasa la utawala huo, na kadiri hali hiyo inavyoendelea ndivyo utawala huo unavyozidi kukaribia kwenye kaburi la maangamizi. Bila ya shaka ni kwa kuzingatia yote hayo ndio maana wachambuzi wa mambo wakauita mwaka huu wa 2017 kuwa ni mwaka wa kushtadi migogoro ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Amma jambo la kulitilia maanani hapa ni kwamba, njama za utawala wa Kizayuni za kuendeleza siasa zake za kujipanua na kupenda vita kupitia njia mbalimbali za kisiasa na kidiplomasia bado zinaendelea na walimwengu hadi sasa wanaendelea kushuhudia njama mbalimbali za utawala huo ghasibu. Bila ya shaka njia bora ya kukabiliana na njama hizo za Israel ni kuzidi kuwa macho wananchi wa eneo hili.