Tangu Oktoba, askari wa Israel wameshawaua shahidi Wapalestina 200
Asksari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewaua shahidi Wapalestina 200 tangu ilipoanza Intifadha ya Quds mwezi Oktoba mwaka jana hadi hivi sasa.
Jumuiya ya kitaifa ya familia za mashahidi wa Palestina leo imetoa ripoti inayoeleza kwamba tangu ilipoanza Intifadha ya Quds mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana hadi sasa, Wapalestina 200 wameuliwa shahidi katika maeneo tofauti ya Ufukwe wa Magharibi, Ukanda wa Gaza na vilevile katika mji wa Baitul Muqaddas.
51 miongoni mwa mashahidi hao ni watoto wadogo na 20 ni wanawake.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika muda wa saa 48 zilizopita Wapalestina saba wameuawa shahidi, watano huko Baitul Muqaddas na wawili katika eneo la Ufukwe wa Magharibi.
Tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka uliopita wa 2015 hadi sasa maeneo mbalimbali ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu yamekuwa yakishuhudia wimbi la malalamiko ya upinzani dhidi ya siasa za kichokozi za utawala wa Kizayuni na njama za utawala huo za kupotosha utambulisho wa Baitul Muqaddas pamoja na mpango wake wa kuugawa kiwakati na kimahali msikiti mtukufu wa Al-Aqsa. Wimbi hilo la malalamiko limekuwa maarufu kwa jina la Intifadha ya Quds.../