Hania: Ahadi ya kukombolewa mateka wote wa Palestina itatimia karibuni hivi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i28088-hania_ahadi_ya_kukombolewa_mateka_wote_wa_palestina_itatimia_karibuni_hivi
Naibu Mkuu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, ahadi ya kukombolewa mateka wote wa Palestina wanaoshikiliwa katika korokoro za utawala ghasibu wa Israel itatimia hivi karibuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 21, 2017 23:14 UTC
  • Hania: Ahadi ya kukombolewa mateka wote wa Palestina itatimia karibuni hivi

Naibu Mkuu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, ahadi ya kukombolewa mateka wote wa Palestina wanaoshikiliwa katika korokoro za utawala ghasibu wa Israel itatimia hivi karibuni.

Ismail Hania amewaambia watu wa Ukanda wa Gaza kwamba mapambano ya mateka wa Palestina katika jela za Israel ni mapambano ya Wapalestina wote na kuongeza kuwa, mapambano ya ukombozi wa Palestina yanasonga mbele tena kwa nguvu na kasi kubwa zaidi ya ilivyokuwa huko nyuma. 

Ismail Hania amesisitiza kuwa, vita vya kiusalama vinaendelea kwa nguvu kubwa na kwamba taasisi za usalama za Ukanda wa Gaza zina uwezo wa kuwafuatilia na kuwatia nguvuni wahalifu wa Kizayuni.

Naibu Mkuu wa Idara ya Siasa ya Hamas amesema kuwa, vibaraka wanaofanya njama dhidi ya eneo la Ukanda wa Gaza wamedhoofika na kwamba eneo hilo litashinda na litaendelea kusimama imara mbele ya mzingiro wa kidhalimu wa utawala haramu wa Israel.

Baada ya harakati ya Hamas kushinda uchaguzi wa Bunge la Palestina uliofanyika mwama 2006, Israel ililizingira eneo la Gaza kutoka pande zote za anga, nchi kavu na baharini kwa shabaha ya kuiondoa madarakani serikali ya harakati hiyo. Utawala huo ghasibu unaendelea kuwazingira watu wa eneo hilo licha ya upinzani mkali wa jamii ya kimataifa.