Wanazuoni Bahrain: Hukumu dhidi ya Sheikh Qassim ni tangazo la vita
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i29390-wanazuoni_bahrain_hukumu_dhidi_ya_sheikh_qassim_ni_tangazo_la_vita
Wanazuoni wa Kiislamu nchini Bahrain wamelaani vikali hatua ya utawala wa Aal-Khalifa kumhukumu msomi mtajika nchini humo Sheikh Issa Qassim kifungo cha mwaka mmoja na kusisitiza kuwa hukumu hiyo ni sawa na tangazo la vita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 21, 2017 09:12 UTC
  • Wanazuoni Bahrain: Hukumu dhidi ya Sheikh Qassim ni tangazo la vita

Wanazuoni wa Kiislamu nchini Bahrain wamelaani vikali hatua ya utawala wa Aal-Khalifa kumhukumu msomi mtajika nchini humo Sheikh Issa Qassim kifungo cha mwaka mmoja na kusisitiza kuwa hukumu hiyo ni sawa na tangazo la vita.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili na wanazuoni wa Bahrain imesema hukumu hiyo dhidi ya msomi na mwanaharakjati huyo wa Kiislamu nchini humo sio ya kiuadilifu na kwamba ni sawa na tangazo la vita.

Kadhalika wanazuoni wa Kiislamu nchini humo wamewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi mabarabarani kuonesha hamasa nyingine ya kuihami dini yao na kumuunga mkono Ayatullah Issa Qassim.

Wakati huo huo, chama cha Kiislamu cha al-Wifaq cha Bahrain sambamba na kukosoa hukumu hiyo, kimesema kupandishwa kizimbani Ayatullah Sheikh Isa Qassim ni sawa na utawala wa Aal-Khalifa kuwafikisha kizimbani na kuwalenga Waislamu wote wa madhehebu ya Shia nchini humo. 

Maandamano ya wananchi ya kulaani hukumu dhidi ya Ayatullah Qassim

Mbali na Sheikh Isa Qassim, mahakama ya Bahrain hii leo imewahukumu pia kifungo cha mwaka mmoja jela kila mmoja, wapambe wa mwanazuoni huyo, Hussein al-Qassab na Mirza al-Dirazi, waliokuwa wakifanya kazi katika ofisi yake.

Bahrain ilikuwa imepanga kusoma hukumu hiyo tarehe saba mwezi huu wa Mei, lakini ikilazimika kuiakhirisha kwa kuhofia hasira za wananchi.