Utawala wa Kizayuni waipongeza Saudia kwa kukata uhusiano na Qatar
(last modified Tue, 06 Jun 2017 08:08:15 GMT )
Jun 06, 2017 08:08 UTC
  • Utawala wa Kizayuni waipongeza Saudia kwa kukata uhusiano na Qatar

Waziri wa Vita wa utawala haramu wa Israel amekaribisha hatua ya Saudi Arabia na baadhi ya nchi za Kiarabu ya kukata mahusiano yao na taifa la Qatar na kusema kuwa, hiyo ni fursa pekee kwa ajili ya Israel.

Avigdor Lieberman sambamba na kufurahishwa na uhusiano uliyopo baina ya Israel na nchi hizo zilizotangaza kukata mahusiano na Qatar hapo jana zikiongozwa na Riyadh, amesema kuwa, mwenendo huo ni fursa muhimu sana kwa ajili ya Israel. Naye Yisrael Katz, Waziri wa Intelejensia wa Israel ameandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba, ukatwaji mahusiano wa baadhi ya nchi za Kiarabu na Qatar ni ukweli mpya wenye changamoto. Naye Eli Avidar, mkuu wa zamani wa wafanyakazi wa ubalozi wa Kizayuni mjini Doha, Qatar amewataka viongozi wa Israel kuharakisha kufikia malengo ya utawala huo katika ardhi za Palestina kwa kutumia mgogoro ulioibuka baina ya Qatar na Saudia.

Viongozi wa nchi zilizokata mahusiano na Qatar

Saudia, Imarat, Bahrain na Misri zilitangaza Jumatatu ya jana hatua yao ya kukata mahusiano ya kidiplomasia na Qatar kwa madai kuwa, Doha inaunga mkono ugaidi, kuingilia mambo ya ndani ya nchi za Kiarabu, kutishia usalama wa kitaifa na kutoa hifadhi kwa magenge ya kigaidi. Kufuatia hali hiyo, jioni ya jana Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Bahram Qassemi alisema kuwa, utatuzi wa tofauti zilizopo baina ya nchi za Mashariki ya Kati utafikiwa kupitia njia ya kisiasa na mazungumzo yenye nia njema.

Yisrael Katz, Waziri wa Intelejensia wa Israel

Kwa mujibu wa Qassemi, kuendelea mvutano baina ya nchi hizo kunatoa mwanya kwa utawala ghasibu wa Israel uweze kuendelea kujitanua na kupora zaidi ardhi za Wapalestina na kusisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inazitaka nchi za Kiislamu kudhibiti hasira na kutatua matatizo yao kwa busara.

Tags