Iran yatenga bandari tatu kuipelekea chakula Qatar
(last modified Thu, 08 Jun 2017 17:55:48 GMT )
Jun 08, 2017 17:55 UTC
  • Muhammed bin Abdul Rahman Aal Thani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar
    Muhammed bin Abdul Rahman Aal Thani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar

Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Muhammed bin Abdul Rahman Aal Thani amesema kuwa, Tehran imetenga bandari zake tatu kwa ajili ya kupeleka chakula nchini Qatar.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr, mtandao wa habari wa al Nashra wa nchini Lebanon umemnukuu Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar akisema kuwa, Iran imetangaza iko tayari kusaidia kutuma chakula kwa Qatar.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Iran imetenga bandari tatu kwa ajili ya kuitumia Qatar chakula.

Vile vile amesema, Uturuki imekusudia kutuma askari wake nchini Qatar kwa ajili ya kulinda usalama katika ardhi nzima ya nchi hiyo.

Itakumbukwa kuwa siku ya Jumatatu ya tarehe 5 Juni, 2017, Nchi za Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu yaani Imarati, Bahrain na Misri zilikata uhusiano wao wa kidiplomasia na mahusiano yote wa majini, angani na ardhini na Qatar zikiituhumu nchi hiyo kuwa inaunga mkono ugaidi na kuingilia masuala ya ndani ya nchi hizo.

Hadi hivi sasa nchi nyingine kadhaa za Afrika zmefuta mkondo huo huku nyingine zikipunguza uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar.

Tags