Mwanaharakati wa Saudia: Mapinduzi dhidi ya utawala wa Aal-Saud yanakaribia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i30820-mwanaharakati_wa_saudia_mapinduzi_dhidi_ya_utawala_wa_aal_saud_yanakaribia
Mwanaharakati wa upinzani na msomi mkubwa raia wa Saudia anayeishi nje ya nchi amesema kuwa, mapinduzi muhimu ya kuung'oa utawala wa kifalme wa Aal-Saud nchini humo yanakaribia.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 22, 2017 13:56 UTC
  • Mwanaharakati wa Saudia: Mapinduzi dhidi ya utawala wa Aal-Saud yanakaribia

Mwanaharakati wa upinzani na msomi mkubwa raia wa Saudia anayeishi nje ya nchi amesema kuwa, mapinduzi muhimu ya kuung'oa utawala wa kifalme wa Aal-Saud nchini humo yanakaribia.

Saad Al-Dosari ameazungumzia hatua ya Mfalme Salman bin Abdul Aziz ya kumuuzulu Mohammed bin Nayef aliyekuwa mrithi wa kiti cha ufalme na kumteua mwanaye, Mohammad bin Salman kuwa mrithi wake na kusema kuwa, ni suala lisilo na shaka yoyote kwamba sasa mapinduzi ya kweli ya kuuondoa madarakani utawala huo wa kifalme nchini Saudia yamekaribia. 

Mohammad bin Salman akiwa na Rais Trump mwenye chuki dhidi ya Uislamu

Al-Dosari ambaye ameyasema hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, sambamba na kumkosoa vikali mwanamfalme huyo mwenye misimamo mikali na kumtaja kwa jina la dubu mwenye hasira na mharibifu, amesema kuwa, mashambulizi ya kikatili yanayofanywa na Mohammad bin Salman nchini Yemen na kadhalika mzingiro wa Saudia dhidi ya Qatar, yalianzishwa na kijana huyo kwa ajili ya kufikia haraka kiti cha ufalme nchini Saudia.

Mohammad bin Salman kulia akiwa na kijana wa Kizayuni na mwasisi wa mtandao wa Facebook

Kabla ya hapo pia katika marasimu ya kutoa baia kwa mrithi mpya wa kiti cha ufalme, Mohammad bin Salman marasimu ambayo yalifanyika katika kasri ya Swafa mjini Makkah na kurushwa moja kwa moja na kanali za habari za Saudia kuanzia al-Arabiayyah, al-Hadath na al-Ikhbariyyah, mwanamfalme mmoja alishindwa kujizuia na kuamua kuonyesha upinzani wake wa wazi mbele ya Bin Salman ambapo alitoa malalamiko yake juu ya uteuzi wake ambao umekinzana na usia wa mwanzilishi wa utawala wa Aal-Saud.