May 09, 2024 07:14 UTC
  • Mgombea wa upinzani Chad alaani vitisho na ghasia dhidi yake na wafuasi wake

Chama cha Succès cha Masra Waziri Mkuu wa Chad ambaye ni mmoja wa wagombea wa urais aliyechuana katika uchaguzi Jumatatu wiki hii jana kililaani ghasia na vitisho dhidi yake na wafuasi wake, na kudai kuwa uchaguzi wa rais uligubikwa na udanganyifu. 

Masra aliye na umri wa miaka 40 ndiye mpinzani mkuu wa Mahamat Idriss Deby Itno Rais wa serikali ya mpito na kiongozi wa kijeshi wa Chad. Uchaguzi wa Rais uliofanyika Jumatatu wiki hii umekusudiwa kuhitimisha miaka mitatu ya utawala wa kijeshi huko Chad hata hivyo wapinzani wa mtawala wa kijeshi wa nchi hiyo walitoa wito wa kususia uchaguzi wakisema kuwa matokeo tayari yameshapangwa.

 

Kiongozi wa mpito wa Chad, Mahamat Idriss Deby 

Chama cha Masra cha The Transformers kilisema katika ukurasa wake wa Facebook kwamba mgombea wake huyo amekuwa akifuatiliwa na kukabiliwa na vitisho. Chama hicho pamoja na Muungano wa Haki na Usawa pia vimelaani vitisho na ghasia kubwa zinazowakabili wafuasi wake ikiwa ni pamoja na kamatakamata kiholela inayoendeshwa na vikosi vya usalama vya Chad dhidi ya wafuasi wake tangu kufanyika uchaguzi wa rais Jumatatu wiki hii.

Chama cha The Transformers cha mpinzani mkuu wa rais wa serikali ya mpito ya Chad kimesema kuwa kimezuiwa kufika katika vituo vya kupigia kura ili kushuhudia zoezi la kuhesabu kura. 

 

Tags