Wazayuni wazidi kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i31406-wazayuni_wazidi_kuvunjia_heshima_matukufu_ya_kiislamu
Katika mwezi uliopita wa Juni, utawala wa Kizayuni wa Israel uliyavunjia heshima mara 80 matukufu ya Kiislamu huko Palestina hususan Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu katika mji wa Quds na Haram na Nabii Ibrahim AS katika mji wa al Khalil
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 06, 2017 07:42 UTC
  • Wazayuni wazidi kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu

Katika mwezi uliopita wa Juni, utawala wa Kizayuni wa Israel uliyavunjia heshima mara 80 matukufu ya Kiislamu huko Palestina hususan Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu katika mji wa Quds na Haram na Nabii Ibrahim AS katika mji wa al Khalil

Shirika la habari la RASA limeripoti kuwa, Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Palestina imetoa tamko na kusema kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel unavunjia heshima kwa makusudi matukufu ya Kiislamu.

Msikiti wa al Aqsa, Kibla cha Kwanza cha Waislamu huko Palestina

 

Tamko la wizara hilo limeongeza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ulizuia mara 40 kusomwa adhana kwenye Msikiti wa al Aqsa katika mwezi uliopita wa Juni.

Katika mwezi huo pia, walowezi 1391 wa Kizayuni walikivamia na kukivunjia heshima Kibla cha Kwanza cha Waislamu huko Palestina.

Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Palestina aidha imesema, katika kipindi cha hivi karibuni, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameongeza kasi ya kuvunjia heshima matukufu ya Waislamu ikiwa ni pamoja na kuongezeka njama za Tel Aviv za kuvuruga muundo wa kijamii, kihistoria na kidini wa mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas.

Wizara hiyo imezitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu kusimama imara kupambana na njama hizo mbaya za Israel.

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Tanzania

Ikumbukwe kuwa mwezi Oktoba 2015, wananchi wa Palestina walianzisha Intifadha ya Quds baada ya kuona walowezi wa Kizayuni kwa ulinzi kamili wa wanajeshi katili wa Israel wamechupa mipaka katika kuvunjia heshima maeneo matakatifu ya Waislamu huko Quds.

Zaidi ya Wapalestina 320 wameshauliwa shahidi na Wazayuni makatili tangu ilipoanza Intifadha hiyo ya Quds na wengine wengi wamejeruhiwa.