Wanajeshi 3 Waisraeli waangamizwa katika Oparesheni ya Mpalestina Quds
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i34879-wanajeshi_3_waisraeli_waangamizwa_katika_oparesheni_ya_mpalestina_quds
Wanajeshi watatu wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameangamizwa katika oparesheni ya kujitolea kufa shahidi ya Mpalestina katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 26, 2017 16:03 UTC
  • Wanajeshi 3 Waisraeli waangamizwa katika Oparesheni ya Mpalestina Quds

Wanajeshi watatu wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameangamizwa katika oparesheni ya kujitolea kufa shahidi ya Mpalestina katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu.

Taarifa zinasema oparesheni hiyo iliyofana imetekelezwa na Mpalestina katika lango la Har Adar la kitongoji cha walowezi wa Kizayuni mapema leo Jumanne. Mpalestina huyo aliyekuwa na umri wa miaka 37 aliwafyatulia risasi wanajeshi Waisraeli na kuwaua kabla ya kuuawa kwa kufyatuliwa risasi.

Wakati huo huo, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, Hamas, na Harakati ya Jihad Islami katika taarifa zimepongeza oparesheni hiyo ya kujitolea kufa shahidi. Jihad Islami imesema oparesheni hiyo ni pigo kubwa kwa wale wanaotaka maelewano na utawala wa Kizayuni wa Israel na kwamba pia inaashiria kuwa hai hisia ya mapambano miongoni wa Wapalestina.

Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds unaokaliwa kwa mabavu na Israel

Harakati ya Hamas nayo imesema oparesheni hiyo ni mwanzo wa mwamko na Intifadha mpya ya Wapalestina. Aidha Hamas imesema oparehseni hiyo imeonyesha kuwa vijana wa Palestina wataendeleza mapamabno hadi ardhi zote za Palestina zitakapokombolewa.

Tokea Oktoba mwaka 2015 wakati wa kuanza Intifadha ya Al Aqsa, Wapalestina karibu 380 wameuawa shahidi baada ya kufyatuliwa risasi na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel.