Wabahrain waandamana kupinga kuanzishwa uhusiano na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i35613-wabahrain_waandamana_kupinga_kuanzishwa_uhusiano_na_israel
Watu wa Bahrain wameandamana kulaani vikali mpango wa ufalme wa nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Oct 13, 2017 12:02 UTC
  • Wabahrain waandamana kupinga kuanzishwa uhusiano na Israel

Watu wa Bahrain wameandamana kulaani vikali mpango wa ufalme wa nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Taarifa zinasema kuwa, maandamano hayo yalifanyika jana Alkhamisi katika miji na vijiji kadhaa vya Bahrain huku wananchi wakitoa nara na kusema, "Hatutaki Uhusiano na Israel."

Waandamanaji hao walitembea juu ya bendera za Marekani na Israel wakitoa nara pia dhidi ya Marekani, ambayo ni muitifaki wa Israel, kwa kusema "Marekani ni Shetani Mkubwa."

Hivi karibuni mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Al Khalifah alinukuliwa na magazeti ya Kizayuni akisema kwamba, wakati umefika kwa nchi za Kiarabu kuwa na uhusiano mzuri na wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mfalme wa Bahrain

Bahrain imejiunga na Saudi Arabia pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu katika kuunga mkono uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unawakandamiza Wapalestina na kuwaangamiza kwa umati. Aidha utawala wa Kizayuni wa Israel unakalia kwa mabavu ardhi za Palestina hasa mji wa Quds ulipo Msikiti wa al Aqswa ambao ni Qibla cha Kwanza cha Waislamu.