Bahrain yataka Qatar ipokonywe uanachama wa baraza la PGCC
Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain, Khalid bin Ahmed Aal Khalifah ametoa mwito wa kuondolewa Bahrain kwenye Baraza la Ushirikiano wa Ghuba ya Uajemi (PGCC).
Bin Ahmed Aal Khalifa ameandika kwenye ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa: Bahrain haitashiriki katika kikao kijacho cha PGCC iwapo Qatar haitabadili misimamo yake kuhusu masuala ya eneo.
Amesema njia bora ya kulibakisha hai Baraza la Ushirikiano wa Ghuba ya Uajemi (PGCC) ni kuiondoa Qatar kwenye taasisi hiyo kubwa ya nchi za Kiarabu.
Hii ni katika hali ambayo, mwezi uliopita wa Septemba, Mfalme Hamad bin Isa Aal Khalifa wa Bahrain alizitaka nchi za Kiarabu kuacha kuusussia utawala haramu wa Israeli sambamba na kutaka kuanzishwe uhusiano kamili wa kidiplomasia baina ya Waarabu na Tel Aviv.
Mapema jana Amir wa Qatar, Tamim Bin Hamad al-Thani alionya kuwa, hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi italitumbukiza eneo zima la Mashariki ya Kati katika machafuko.
Ifahamike kuwa, Saudi Arabia, Imarati, Bahrain na Misri tarehe 5 Juni mwaka huu zilitangaza kukata uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar zikiituhumu Doha kuwa inaunga mkono ugaidi, madai ambayo yamekabidhibishwa vikali na serikali ya Doha.