Saad Hariri: Nitarudi Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i36418-saad_hariri_nitarudi_lebanon
Saad Hariri, Waziri Mkuu wa Lebanon aliyejiuzulu amesema kuwa atarejea nchini humo kama alivyotamka hapo awali.
(last modified 2026-05-19T09:45:50+00:00 )
Nov 15, 2017 11:57 UTC
  • Saad Hariri: Nitarudi Lebanon

Saad Hariri, Waziri Mkuu wa Lebanon aliyejiuzulu amesema kuwa atarejea nchini humo kama alivyotamka hapo awali.

Saad Hariri ameyasema hayo baada ya Rais Michel Aoun wa Lebanon kusema hii leo kuwa hakuna kitu chochote kinachohalalisha kushindwa kurejea nchini Hariri baada ya kupita siku 12 tangu ajiuzulu  na kwamba Lebanon inamtambua Hariri kama mtu aliyetiwa mbaroni; hatua inayokinzana na makubaliano ya Vienna. 

Rais Michel Aoun wa Lebanon 

Rais wa Lebanon amebainisha kuwa nchi hiyo imechukua hatua za lazima kwa ajili ya kurejea nchini Saad Hariri na kwamba hawakubali Hariri awe mateka. Rais Michel Aoun amesema, anathibitisha kwamba familia ya Hariri pia iko chini ya udhibiti nchini Saudi Arabia na kwamba familia hiyo inapekuliwa wakati wa kuingia na kutoka nyumbani. Saad Hariri alitangaza kujiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu wa Lebanon tarehe Nne mwezi huu kupitia ujumbe alioutuma kwa njia ya video kutokea nchini Saudia na hadi sasa bado hajarejea Lebanon.