Harakati ya Ansarullah yavionya baadhi ya vyama vinavyovuruga usalama wa Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i37063-harakati_ya_ansarullah_yavionya_baadhi_ya_vyama_vinavyovuruga_usalama_wa_yemen
Harakati yya Ansarullah ya Yemen imetahadharisha kuhusiana na njama za baadhi ya vyama zinazolenga kuvuruga amani na usalama wa nchi hityo inayokabiliwa na hujuma na mashambulio ya kiijeshi ya Saudi Arabia na washirika wake.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 02, 2017 04:35 UTC
  • Harakati ya Ansarullah yavionya baadhi ya vyama vinavyovuruga usalama wa Yemen

Harakati yya Ansarullah ya Yemen imetahadharisha kuhusiana na njama za baadhi ya vyama zinazolenga kuvuruga amani na usalama wa nchi hityo inayokabiliwa na hujuma na mashambulio ya kiijeshi ya Saudi Arabia na washirika wake.

Harakati ya Wananchi ya Ansarullah ya Yemen imesema katika taarifa yake kwamba,  akthari ya wananchi wa Yemen wanasisitiza juu ya kutekelezwa Katiba na kukabiliana na aina yoyote ile ya upotoshaji na uvurugaji amani na usalama wa nchi hiyo.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeeleza kuwa, kuvuruga amani na usalama wa nchi hiyo ni jambo hatari mno na kwamba, kuna baadhi ya makundi ambayo yamekuuwa yakivishambulia vikosi vya usalama vya nchi hiyo. 

Hayo yanajiri katika hali ambayo, mashambulio na hujuma ya kijeshi ya Saudi Arabia na washirika wake ingali inaendelea huko nchini Yemen hukuu tahadhari za kuutokea maafa ya kibinadamu nazo zikitolewa na mashirika mbalimbali ya kibinadamu.

Yemen inavyobomolewa na mashambulio ya Saudia

Saudia kwa uungaji mkono wa Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel, Imarati na baadhi ya nchi za Kiarabu, ilianzisha mashambulizi ya kikatili ya pande zote dhidi ya wananchi wa Yemen mwezi Machi 2015. Hata hivyo muqawama wa wananchi Waislamu wa Yemen umewatumbukiza kwenye kinamasi kikubwa wavamizi hao ambao hivi sasa wanaanza kugombana wao kwa wao.

Maelfu ya Wayemeni wameuawa na mamilioni ya wengine kulazimika kuwa wakimbizi kutokana na mashambulizi hayo ya Saudi Arabia ikiungwa mkono na Marekani, Israel na nchi nyingine kadhaa dhidi ya taifa la Yemen. Mashambulizi hayo makali yanaendelea kwa mwaka wa tatu sasa.