Ansarullah yasema imezima tishio kuu kwa usalama wa Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i37201-ansarullah_yasema_imezima_tishio_kuu_kwa_usalama_wa_yemen
Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema harakati hiyo imefanikiwa kutibua tishio kuu kwa usalama wa nchi hiyo, kwa kuzima njama zilizoliwa na rais wa zamani wa nchi hiyo aliyeuawa hapo jana, Ali Abdullah Saleh na vikosi vitiifu kwake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 05, 2017 04:28 UTC
  • Ansarullah yasema imezima tishio kuu kwa usalama wa Yemen

Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema harakati hiyo imefanikiwa kutibua tishio kuu kwa usalama wa nchi hiyo, kwa kuzima njama zilizoliwa na rais wa zamani wa nchi hiyo aliyeuawa hapo jana, Ali Abdullah Saleh na vikosi vitiifu kwake.

Abdulmalik al-Houthi amesema licha ya kujificha nyuma ya pazia na hadaa kwamba anapinga vikali uvamizi wa Saudi Arabia nchini humo, lakini Saleh hatimaye alidhihirisha sura yake halisi na kuanza kushirikiana na wavamizi hao.

Al-Houthi amesema, na hapa tunanukuu: "Tuwalionya dhidi ya kuchochea vita na kujihusisha na vitendo vya jinai, lakini wakakataa kutusikiliza, huku wakishupalia kutekeleza maagizo ya Saudia ya kufunga barabara zote muhimu za mji mkuu Sana'a." Mwisho wa kunukuu.

Kiongozi wa Ansarullah wa Yemen amesema harakati hiyo imefanikiwa kuzima njama hizo, kwa kuwa vikosi hivyo vitiifu kwa Abdallah Saleh vilikusudia kuuteka Sana'a, na kisha miji na mikoa mingine ya Yemen.

Wanamapambano wa Ansarullah wa Yemen

Amebainisha kuwa, wananchi Waislamu wa Yemen walisimama kidete na kuunga mkono muqawama wa Ansarullah, ndiposa harakati hiyo ya wananchi ikapata mafanikio katika kuzima njama za maadui.

Saleh aliuawa hapo jana wakati alipokuwa akikimbia kutoka mjini San'a kuelekea Ma'rib.

Vikosi vya usalama vya Yemen jana Jumatatu viligundua njia aliyokuwa anatumia Ali Abdullah Saleh kutoka eneo moja hadi jingine na walipata taarifa za kiitelijinsia za namna wafuasi wake walivyokuwa wanapanga kumtorosha San'aa na kumkimbiza mafichoni Ma'rib.

Abdallah Saleh kabla ya kuuawa