Israel yaunga mkono rasmi ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i38959-israel_yaunga_mkono_rasmi_ugaidi
Mkuu wa kamati ya kushughulikia suala la mateka na Wapalestina wanaoachiliwa huru amesema kuwa, utawala wa Kizayuni unawasaidia kifedha Wazayuni wanaofanya jinai dhidi ya wananchi wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 14, 2018 10:31 UTC
  • Israel yaunga mkono rasmi ugaidi

Mkuu wa kamati ya kushughulikia suala la mateka na Wapalestina wanaoachiliwa huru amesema kuwa, utawala wa Kizayuni unawasaidia kifedha Wazayuni wanaofanya jinai dhidi ya wananchi wa Palestina.

Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB limemnukuu Isa Qaraqa, mkuu wa kamati ya kushughulikia suala la mateka na Wapalestina wanaochiliwa huuru akisema kuwa, utawala wa Kizayuni umetenga fedha nyingi za kuwasaidia na kuwaunga mkono Wazayuni wanaofungwa kwa kufanya jinai dhidi ya Wapalestina.

Bendera ya utawala wa Kizayuni wa Israel

 

Amesisitiza kuwa, utawala pandikizi wa Israel unaunga mkono rasmi ugaidi na mauaji si ndani ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu tu, bali hata nje ya ardhi hizo.

Afisa huyo wa Palestina ameongeza kuwa, Israel inafanya jinai kubwa dhidi ya wananchi wa Palestina zikiwemo za ubaguzi wa kizazi na pia kupitisha sheria za kidhalimu na za kibaguzi inazozizusha kila siku.

Itakumbukwa kuwa hivi sasa kuna karibu Wapalestina 7000 wanaoishi katika mazingira mabaya sana kwenye jela za kutisha za utawala wa Kizayuni wa Israel ambapo 350 kati yao ni watoto wadogo na 12 ni wabunge wa Palestina.