Kushtadi jinai za Wazayuni dhidi ya watoto wa Kipalestina
(last modified Mon, 29 Jan 2018 04:36:19 GMT )
Jan 29, 2018 04:36 UTC
  • Kushtadi jinai za Wazayuni dhidi ya watoto wa Kipalestina

Wanajeshi wa utawala haramu wa Kizayuni wamewauwa shahidi watoto watatu wa Kipalestina tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2018 hadi sasa.

Wizara ya Habari ya Palestina imetangaza kuwa watoto wa Kipalestina 52 wametiwa mbaroni na wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni mwezi huu wa Januari katika Ukanda wa Ghaza, Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan na Quds mashariki. 

Wizara hiyo imesema, viongozi wa utawala wa Kizayuni wamezidisha hatua za kukiuka sheria kuhusiana na watoto wa Kipalestina katika maeneo yote ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo dhalimu.  

Wanajeshi wa Israel wakiwatia mbaroni kwa mabavu watoto wa Kipalestina 
 

Taarifa ya wizara hiyo imeongeza kuwa, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wamezidisha hatua zao za kukiuka haki za watoto wa Kipalestina baada ya wananchi wa Palestina kusimama kidete kutangaza malalamiko na kufanya maandamano ya kupinga uamuzi wa rais wa Marekani, Donald Trump wa kuitangaza Quds kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni. 

Wizara ya Habari ya Palestina imeripoti kuwa mwaka jana wa 2017 wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni waliwauwa shahidi watoto 17 wa Kipalestina na kuwatia mbaroni wengine 1,620. Wizara hiyo imebainisha kuwa, watoto wengine 350 wa Kipalestina wanashikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni. 

Tags