Viongozi wa Lebanon wasema Israel ni tishio kwa usalama mpakani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i40001-viongozi_wa_lebanon_wasema_israel_ni_tishio_kwa_usalama_mpakani
Viongozi watatu wa ngazi za juu nchini Lebanon wamesema utawala haramu wa Israel ni tishio kwa uthabiti wa eneo la mpakani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 06, 2018 10:47 UTC
  • Viongozi wa Lebanon wasema Israel ni tishio kwa usalama mpakani

Viongozi watatu wa ngazi za juu nchini Lebanon wamesema utawala haramu wa Israel ni tishio kwa uthabiti wa eneo la mpakani.

Kauli hiyo imekuja baada ya utawala haramu wa Israel kutoa vitisho baada ya Lebanon kutangaza zabuni za kimataifa za uchimbaji mafuta na gesi katika mipaka yake ya Bahari ya Mediterranean.

Rais Michel Aoun, Waziri Mkuu Saad al-Hariri na Spika wa Bunge Nabih Berri wameafiki kuchukua hatua kuzuia utawala hramu wa Israel kujenga ukuta baina ya Lebanon na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Uchimbaji mafuta baharini

Aidha viongozi hao watatu wa Lebanon wamesema watachukua hatua kukabiliana na vitisho vya Israel kuhusu uchimbaji mafuta na gesi.

Wiki iliyopita, Waziri wa Vita wa Utawala wa Kizayuni wa Israel Avidgor Lieberman alitoa vitisho baada ya Lebanon kutangaza zabuni za uchimbaji mafuta na gesi katika eneo la mipaka yake ya Bahari ya Mediterranean. Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel usithubutu kutoa vitisho kwa Lebanon.