Bashar Assad aafiki uchaguzi wa mapema Syria
Rais wa Syria ametangaza kuwa serikali ya nchi hiyo iko tayari kwa ajili ya kufanyika uchaguzi wa rais wa mapema.
Rais Bashar al Assad wa Syria amesema kuwa yuko tayari uchaguzi wa rais wa nchi hiyo ufanyike mapema kabla ya wakati, iwapo wananchi watataka iwe hivyo.
Rais wa Syria amesisitiza kuwa suala la kufanyika uchaguzi wa mapema kabla ya wakati wake halikujumuishwa katika mchakato wa sasa wa kisiasa wa nchi hiyo, na kwamba ni bora rais achaguliwe moja kwa moja na wananchi na si bunge. Amesema suala hilo linahitaji maoni ya Wasyria wenyewe, na si maoni ya serikali au rais.
Rais Assad ameongeza kuwa katika mazingira ya sasa kipaumbele cha kwanza ni kutekekeza na kulinda makubaliano ya kusitisha vita na kwamba yuko tayari kumpokea mwanamgambo yoyote atakayeweka chini silaha yake ili kuzuia kumwagika damu huko Syria. Syria ilikumbukwa na mgogoro tangu mwaka 2011 sambamba na kushadidi hujuma na mashambulizi ya makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono kwa hali na mali na Marekani na waitifaki wake, lengo kuu likiwa ni kuing'oa madarakani serikali halali ya Bashar al Assad.