Ripoti: Mohammad Bin Salman anapanga kuhamisha vita kutoka Yemen kwenda Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i43736-ripoti_mohammad_bin_salman_anapanga_kuhamisha_vita_kutoka_yemen_kwenda_lebanon
Gazeti la Lebanon la Al Akhbar Mail limenukuu ujumbe wa mtandaoni wa balozi wa Imarati mjini Washington, Marekani ambao umeonyesha uwepo wa njama kubwa za Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia za kuhamisha vya Yemen kwenda nchini Lebanon.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 27, 2018 23:27 UTC
  • Ripoti: Mohammad Bin Salman anapanga kuhamisha vita kutoka Yemen kwenda Lebanon

Gazeti la Lebanon la Al Akhbar Mail limenukuu ujumbe wa mtandaoni wa balozi wa Imarati mjini Washington, Marekani ambao umeonyesha uwepo wa njama kubwa za Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia za kuhamisha vya Yemen kwenda nchini Lebanon.

Taarifa ya gazeti hilo la Al Akhbar Mail limefichua ujumbe wa Yousef Al Otaiba, balozi wa Imarati nchini Marekani akimnukuu Abdulrahman Al Sad'han, mshauri wa Bin Salman akimtaka mrithi huyo wa kiti cha ufalme wa Saudia kuhamisha vita hiyo kutoka Yemen kwenda Lebanon.

Yousef Al Otaiba, balozi wa Imarati nchini Marekani

Ujumbe huo umeashiria pia vitisho dhidi ya Saad Hariri, Waziri Mkuu wa Lebanon alipokamatwa mjini Riyadh kwa kisingizio cha miamala yake ya kifedha. Hata hivyo gazeti hilo limeahidi kuchapisha maelezo yote ya ujumbe huo wa balozi wa Imarati naye akimnukuu mshauri wa mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia. Kutokana na vita vya Yemen kuchukua muda mrefu sambamba na kutofikia natija yoyote, kuibuka mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi nne za Kiarabu zikiongozwa na Saudia dhidi ya Qatar na kadhalika suala la kujiuzulu Saad Hariri, Waziri Mkuu wa Lebanon ambalo hata hivyo liligonga ukuta, Riyadh imehisi kushindwa kila upande katika mipango yake.

Abdulrahman Al Sad'han, mshauri wa Bin Salman

Hariri alitangaza kujiuzulu mwezi Novemba mwaka jana baada ya kufanya safari ya ghafla mjini Riyadh na kutoa maneno makali dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Harakati ya Hizbullah. Hata hivyo mwezi mmoja baadaye alibatilisha tangazo lake hilo. Matukio hayo yamewafanya Walebanon walio wengi kuamini kwamba hadi sasa Saudia bado inaendeleza mashinikizo dhidi ya serikali ya Beirut kwa lengo la kuipigisha magoti nchi hiyo na kuilazimisha ifuate amri zake.