Makumi ya magaidi nchini Syria wajisalimisha
Makumi ya magaidi nchini Syria wameripotiwa kujisalimisha kwa jeshi la nchi hiyo ikiwa ni kuzidi kupata pigo magaidi hao na waungaji mkono wao.
Taarifa iliyotolewa na eshi la Syria imeelerza kuwa, magaidi wasiopungua 156 wamejisalimisha kwa jeshi kaskazini mwa mji wa Homs.
Imeelezwa kuwa, magaidi hao wamelazimika kujisalimisha baada ya kuzingirwa kila upande na jeshi la Syria.
Kwa siku kadhaa sasa eneo la kaskazini mwa mkoa wa Homs na kusini mwa mkoa wa Hama mikoa ambayo iko kaskazini mwa Syria kumekuwa kukifanyika mazungumzo ya kuondoka magenge ya kigaidi katika maeneo hayo.
Sambamba na kujisalimisha makumi ya magaidi wa Syria, kikosi maalumu cha jeshi la nchi hiyo kimeelekea katika mji wa Hama kwa shabaha ya kuwasafisha kikamilifu magaidi katika mji huo.
Aidha baadhi ya ripoti zinasema kuwa, vitongoji vya kusini mwa mji mkuu Damascus na katika njia inayoelekea katika Haram Tukufu ya Bibi Zaynab AS vimo mbioni kusafishwa kikikamilifu na uwepo wa makundi ya kigaidi wanaopata uungaji mkono wa madola ya Magharibi na baadhi ya nchi za Kiarabu.
Tokea mwaka 2011, Syria imekumbwa na hujuma kubwa ya magaidi wanaopata himaya ya Marekani, Saudi Arabia na baadhi ya waitifaki wao katika eneo hili kwa lengo la kuvuruga mlingano wa kieneo kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Hata hivyo kusimama kidete wananchi, serikali na jeshi la Syria kumekwamisha njama hizo.