Walowezi wa Kizayuni wauhujumu Msikiti wa Al Aqsa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i43858-walowezi_wa_kizayuni_wauhujumu_msikiti_wa_al_aqsa
Makumi ya walowezi wa Kizayuni leo asubuhi Jumatatu wameuhujumu Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Apr 30, 2018 09:24 UTC
  • Walowezi wa Kizayuni wauhujumu Msikiti wa Al Aqsa

Makumi ya walowezi wa Kizayuni leo asubuhi Jumatatu wameuhujumu Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Kwa mujibu wa Kituo cha Habari cha Palestina, magenge kadhaa ya walowezi wa Kizayuni, wakiwa wanapata himaya ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameuhujumu Msikiti wa Al Aqsa kupitia lango la Al Maghariba. Walowezi hao wa Kizayuni walirandaranda katika uwanja wa msikiti huo huku wakiuvunjia heshima.

Msikiti wa Al Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu, ni nembo muhimu ya utambulisho wa Kiislamu na Kipalestina katika mji wa Quds na walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakilihujumu eneo hilo takatifu mara kwa mara. Lengo la hujuma na uchokozi huo wa Wazayuni wanaopata himaya ya utawala wa Kizayuni wa Israel ni kuharibu utambulisho wa Kiislamu na Kikristo wa Quds Tukufu na badala yake kuweka nembo bandia za Kizayuni.

Mji wa Quds

Katika upande mwingine, Bunge la Utawala wa Kizayuni (Knesset) leo limepitisha sheria ambayo inasema mitaa ya makaazi itajengwa tu kwa ajili ya Mayahudi katika hali ambayo hata kamati ya kisheria ya bunge hilo ilikuwa imesema sheria kama hiyo ni ya kibaguzi.

Taasisi za kutetea haki za Waarabu huko Israel kwa miaka kadhaa sasa zimekuwa zikilalamika kuwa Waarabu wanaoishi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel, ambao ni takribani milioni moja na nusu, hawana haki ya kumiliki nyumba katika baadhi ya mitaa na kwamba haki ya umiliki ni ya Wazayuni tu.