Amnesty International: Israel lazima iwekewe vikwazo vya silaha
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i44020-amnesty_international_israel_lazima_iwekewe_vikwazo_vya_silaha
Shirika la Kimataifa la Msamaha Duniani jana usiku lilionesha kukasirishwa sana na jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Palestina na kuzitaka nchi za dunia ziiwekee vikwazo vya silaha Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 04, 2018 02:48 UTC
  • Amnesty International: Israel lazima iwekewe vikwazo vya silaha

Shirika la Kimataifa la Msamaha Duniani jana usiku lilionesha kukasirishwa sana na jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Palestina na kuzitaka nchi za dunia ziiwekee vikwazo vya silaha Israel.

Hatua hiyo ya Amnesty International imechukuliwa baada ya utawala wa Kizayuni kuwaua shahidi na kuwajeruni maelfu ya Wapalestina wanaofanya maandamano ya kupigania haki yao ya kimsingi ya kurejea wakimbizi wao katika ardhi zao za jadi.

Naibu Mkurugenzi wa Amnesty International katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini amesema, katika wiki zilizopita, dunia imeona namna Israel inavyofanya mashambulizi ya kinyama na kuwadungua kwa risasi raia wa Palestina wanaofanya maandamano ya amani, hivyo kuna wajibu wa kuwekewa vikwazo vya silaha Israel.

Wapalestina wakikabiliana na jinai za Israel wakiwa mikono mitupu bila ya silaha licha ya Wazayuni kukabiliana na Wapalestina hao kwa silaha nzito nzito

 

Maandamano hayo ya wananchi wa Palestina yalianza tarehe 30 Machi mwaka huu kwa mnasaba wa kuadhimisha "Siku ya Ardhi."

Tangu tarehe 30 Machi hadi tarehe 4 Mei, Wapalestina 50 wameshauawa shahidi kwa kupigwa risasi za kivita na wanajeshi katili wa Israel na zaidi ya 7000 wengine wameshajeruhiwa.

Nchi nyingi duniani ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na taasisi mbalimbali za kimataifa zimekuwa zikilaani mfululizo jinai hizo za Wazayuni.

Israel inaendelea kuteka ardhi za Wapalestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni lengo na shabaha yake kuu ikiwa ni kulifuta kabisa taifa la Palestina katika uso wa dunia.