Hamas: Mapambano yataendelea hadi pale utawala wa Kizayuni utakapoangamizwa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i44156-hamas_mapambano_yataendelea_hadi_pale_utawala_wa_kizayuni_utakapoangamizwa
Kiongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, mapambano dhidi ya adui Mzayuni yataendelea mpaka pale utawala wa Kizayuni wa Israel utakapoangamizwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 07, 2018 02:12 UTC
  • Hamas: Mapambano yataendelea hadi pale utawala wa Kizayuni utakapoangamizwa

Kiongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, mapambano dhidi ya adui Mzayuni yataendelea mpaka pale utawala wa Kizayuni wa Israel utakapoangamizwa.

Dakta Mahmoud al-Zahar amesema hayo katika shughuli ya kusindikiza maiti za mashahidi wa Kipalestina waliouawa shahidi hivi karibuni na kusema kuwa, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anatambua kwamba, mauaji hayo ya jeshi la Israel katu hayawezi kudhoofisha irada ya wananchi wa Palestina.

Afisa huyo mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina  amesisitiza kwamba, kwa hali yoyote ile wananchi wa Palestina wataendelea na muqawama na mapambano yao dhidi ya Wazayuni maghasibu hadi watakapopata ushindi.

Ameongeza kuwa, Wapalestina wana imani na ushindi na kwamba, iko siku watafanikiwa kuuushinda utawala ghasibu wa Israel unaozikalia kkwa mabavu ardhi zao.

Wanamapambano wa Hamas

Kuhusiana na maandamano ya 'Haki ya Kurejea', mjumbe huyo wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, maandamano hayo yamekwamisha mipango kama 'Mapatano ya Karne'.

Juzi Jumamosi wanamuqawama sita wa brigedi ya Izzuddin Qassam tawi la kijeshi la harakati ya Hamas waliuawa shahidi na wengine watatu walijeruhiwa katika mripuko mkubwa wa bomu uliotokea katikati ya Ukanda wa Gaza.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeeleza kupitia taarifa yake kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ndio uliohusika na mripuko huo.