Utawala wa Israel unashirikiana na Saudia katika kuwaua watu wa Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i44966-utawala_wa_israel_unashirikiana_na_saudia_katika_kuwaua_watu_wa_yemen
Ndege za kivita za Utawala wa Kizayuni wa Israel aina ya F-35 zinashiriki katika hujuma inayoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya watu wa Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 25, 2018 09:25 UTC
  • Utawala wa Israel unashirikiana na Saudia katika kuwaua watu wa Yemen

Ndege za kivita za Utawala wa Kizayuni wa Israel aina ya F-35 zinashiriki katika hujuma inayoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya watu wa Yemen.

Amikam Norkin Kamanda wa Jeshi la Anga la Utawala wa Kizayuni wa Israel amenukuliwa akijigamba kuwa Israel imetumia ndege hizo za kisasa  za Kimarekani aina ya F-35 katika kushambulia maeneo mawili Asia Magharibi au Mashariki ya Kati. Duru zinadokeza kuwa mbali na kutumia ndege hizo katika kuihujumu Syria, Israel pia imezitumia katika kuisaidia Saudi Arabia katika vita vyake dhidi ya watu wa Yemen. Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti kuwa kumekuwepo na ushirikiano wa karibu wa kijeshi baina ya Saudia na Israel hasa katika vita dhidi ya Yemen. 

Utawala wa Kizayuni wa Israel mwaka 2010 ulitia saini mkataba wa kununua ndege 50 za kivita aina ya F-35 kutoka Marekani na hadi sasa imepokea ndege tisa.

Ndege ya kivita aina ya F-35

Utawala wa Kizayuni wa Israel unashirikiana na Saudi Arabia katika kuishambulia nchi masikini zaidi ya Kiarabu yaani Yemen. Umoja wa Mataifa umeshindwa kuzia hujuma hiyo ya kinyama iliyoanza Machi mwaka 2015 ambapo hadi sasa zaidi ya Wayemen 14,000, wengi wakiwa ni wanawake na watoto, wameuawa na makumi ya maelfu ya wengine wakijeruhiwa huku mamilioni wakifanya kuwa wakimbizi.