Israel yahamakishwa na jibu kali lililotolewa na wanamuqawama wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i45184-israel_yahamakishwa_na_jibu_kali_lililotolewa_na_wanamuqawama_wa_palestina
Jibu kali lililotolewa na muqawama wa Palestina kufuatia jinai za kila mara za askari wa Kizayuni la kuvurumisha makombora 22 kulenga kambi kadhaa za utawala huo, limemkasirisha Waziri wa Sheria wa Utawala Haramu wa Israel na kumfanya atishie kwamba ili kutoa pigo kwa uongozi wa muqawama machaguo yote yako mezani hususan la kuvamia na kulikalia kwa mabavu eneo la Ukanda wa Gaza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 30, 2018 10:38 UTC
  • Israel yahamakishwa na jibu kali lililotolewa na wanamuqawama wa Palestina

Jibu kali lililotolewa na muqawama wa Palestina kufuatia jinai za kila mara za askari wa Kizayuni la kuvurumisha makombora 22 kulenga kambi kadhaa za utawala huo, limemkasirisha Waziri wa Sheria wa Utawala Haramu wa Israel na kumfanya atishie kwamba ili kutoa pigo kwa uongozi wa muqawama machaguo yote yako mezani hususan la kuvamia na kulikalia kwa mabavu eneo la Ukanda wa Gaza.

Ayelet Shaked ameyasema hayo katika mahojiano na moja ya redio za utawala huo katili katika radiamali ya mashambulizi ya makombora ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS kuelekea vitongoji kadhaa vilivyoko karibu na Ukanda wa Gaza na kutaka hatua zaidi zichukuliwe na Tel Aviv kwa ajili ya kuishambulia harakati hiyo ya muqawama.

Ayelet Shaked, Waziri wa Vyombo vya Sheria wa Utawala Haramu wa Israel

Kabla ya hapo Zeef Elikan jumbe wa baraza la usalama la Israel pia alitoa matamshi ya kutaka kuendelezwa siasa za kushupalia vita na kujitanua ambapo alitaka kushadidishwa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya eneo la Gaza. Naye Waziri wa Usalama wa Umma, Masuala ya Kistratejia na Habari wa utawala wa Kizayuni Gilad Erdan amenukuliwa akisema kuwa, viongozi wa harakati ya HAMAS hususan Yahya Sinwar, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati hiyo katika Ukanda wa Gaza ni lazima wauawe. Hii ni katika hali ambayo asubuhi ya leo ndege za kivita za utawala huo katili wa Israel zimefanya mashambulizi katika maeneo zaidi ya 20 ya muqawama wa Palestina ya Gaza. Nayo makundi ya muqawama yamejibu mapigo dhidi ya hujuma hizo kwa kuvurumisha makombora kuelekea vitongoji kadhaa vya walowezi wa Kizayuni.

Moja ya makombora ya Harakati ya Muqawama wa Palestina HAMAS

Kwa mujibu wa taarifa hiyo katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, muqawama wa Palestina umevurumisha karibu makombora na maguruneti 130 kuelekea upande wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) ambapo walowezi kadhaa wa Kizayuni wamejeruhiwa vibaya. Hii ni katika hali ambayo tangu kulipoanza maandamano ya Haki ya Kurejea tarehe 30 Machi mwaka huu, askari wa utawala khabithi wa Israel wamewaua shahidi Wapalestina 120 huku ukitekeleza pia mashambulizi dhidi ya ngome za Brigedi ya Izzudeen Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na brigedi za Al-Quds, tawi la kijeshi la harakati ya Jihadul-Islami na kusababisha vifo vya wanamuqawama watatu wa harakati hizo.