Ndege za Israel zinaisaidia Saudia katika hujuma dhidi ya Yemen: Ansarullah
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i45354-ndege_za_israel_zinaisaidia_saudia_katika_hujuma_dhidi_ya_yemen_ansarullah
Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen Sayyid Abdul-Malik Badruddin al-Houthi amefichua kuwa ndege za kivita za utawala haramu wa Israel zimeonekana zikiruka katika anga ya Bandari ya Hudaydah katika Bahari ya Sham nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 03, 2018 10:25 UTC
  • Ndege za Israel zinaisaidia Saudia katika hujuma dhidi ya Yemen: Ansarullah

Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen Sayyid Abdul-Malik Badruddin al-Houthi amefichua kuwa ndege za kivita za utawala haramu wa Israel zimeonekana zikiruka katika anga ya Bandari ya Hudaydah katika Bahari ya Sham nchini humo.

Kiongozi wa Ansarullah amenukuliwa na kanali ya Televisheni ya Al Masirah akisema ndege za kivita za Israel zimeonekana katika anga ya Hudaydah wakati ambao mamluki wa Saudi Arabia wanatekeleza mkakati wa kuuteka mji huo wa kistratijia.

"Uhalisia wa mambo ni kuwa Yemen inakabiliana kivita na muungano wa Wasaudia na Wazayuni," amesema Sayyid Al Houthi akiashiria hujuma ya kijeshi inayoendelezwa na Saudia pamoja na washirika wake dhidi ya Yemen. Nchi kadhaa za Magharibi hasa Marekani na Uingereza zinafahamika kuwa zinaunga mkono Saudia wazi wazi katika vita vyake vilivyo kinyume cha sheria dhidi ya Yemen na kumekuwepo na ripoti kadhaa za ushirikiano wa kisiri wa Saudia na Israel katika vita dhidi ya nchi hiyo masikini zaidi ya Kiarabu.

Watoto ni waathirika wakuu wa hujuma za Saudia dhidi ya Yemen

Israel na Saudi Arabia hazina uhusiano wa kidiplomasia, lakini tawala hizo mbili zimekuwa zikifanya jitihada za nyuma ya pazia kuanzisha uhusiano rasmi.

Ikumbukwe kuwa Saudia ilianzisha hujuma yake dhidi ya Yemen mnamo Machi mwaka 2015 kwa lengo la kuirejesha madarakani serikali kibaraka ya Abdu Rabuh Mansour Hadi aliyejiuzulu urais na kukimbilia mji mkuu wa Saudia, Riyadh, ambapo watu zaidi ya 14,000 wameuawa na mamilioni ya wengine kujeruhiwa. 

Katika kukabiliana na jinai hizo, wanajeshi wa Yemen wamekuwa wakitumia makombora yaliyoundwa nchini humo kushambulia maeneo kadhaa ya kijeshi na kiuchumi ya Saudi Arabia ukiwemo mji mkuu wa nchi hiyo, Riyadh.