Hizbullah: Taifa la Palestina litegemee muqawama, lisiwategemee viongozi wa Kiarabu wanafiki
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i45384-hizbullah_taifa_la_palestina_litegemee_muqawama_lisiwategemee_viongozi_wa_kiarabu_wanafiki
Mjumbe wa Baraza Kuu la Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah, Nabil Qaouk amesisitiza kwamba, taifa la Palestina halitakiwi kuwategemea viongozi wa nchi za Kiarabu na vikao vyao, bali wategemee muqawama na stratijia yake.
(last modified 2026-01-14T11:42:18+00:00 )
Jun 04, 2018 04:16 UTC
  • Hizbullah: Taifa la Palestina litegemee muqawama, lisiwategemee viongozi wa Kiarabu wanafiki

Mjumbe wa Baraza Kuu la Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah, Nabil Qaouk amesisitiza kwamba, taifa la Palestina halitakiwi kuwategemea viongozi wa nchi za Kiarabu na vikao vyao, bali wategemee muqawama na stratijia yake.

Sheikh Nabil Qaouk ameyasema hayo Jumapili ya jana ambapo sambamba na kuashiria juu ya uhusiano wa karibu wa utawala wa Aal-Saud na utawala wa Kizayuni, amesema, harakati ya Hizbullah inaingia katika serikali mpya ya Lebanon ili ndani ya serikali hiyo iweze kushirikiana na marafiki na waitifaki wake katika kusaidia kuchukua maamuzi bora ya kitaifa dhidi ya uingiliaji wa Marekani na Saudia.

Nabil Qaouk, Mjumbe wa Baraza Kuu la Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah

Kadhalika amesisitiza kwamba, ushiriki wa harakati ya Hizbullah katika serikali mpya ya Lebanon, utazuia uingiliaji wa Saudia. Kadhalika Nabil Qaouk amefafanua kwamba, kunyamanzia uingiliaji wa Saudia katika uchaguzi wa bunge nchini Lebanon na hivi sasa katika uundwaji wa serikali nchini Iraq, ni jambo la kufedhehesha, kudhalilisha na ni ufisadi. Mjumbe wa Baraza Kuu la Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ameutaja utawala wa Aal-Saud kuwa ni utawala uliogubikwa na kashfa kwa sababu kila mtu anajua kuwa utawala wa Kizayuni unatekeleza jinai zake dhidi ya raia wa Palestina chini ya kivuli cha njama za Saudia na kwamba taifa la Palestina linalipa gharama kutokana na kujipendekeza kunakofanywa na Wasaudi kwa Marekani na utawala wa Kizayuni.

Mfalme Salman akimvisha mkufu wa dhahabu Rais Donald Trump wa Marekani

Sheikh Nabil Qaouk ameongeza kwa kusema, awali jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina zilitekelezwa kwa sababu ya kimya cha nchi za Kiarabu, lakini hii leo zinatekelezwa kutokana na njama za baadhi ya nchi za Kiarabu.