Waziri wa vita wa Israel atoa vitisho vipya kwa Wapalestina
Waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni ametishia kuwa Israel itamalizia hasira zake kwa harakati za Hamas, Jihadul Islam na makundi yote ya muqawama ya Palestina yanayoendesha mapambano dhidi ya utawala vamizi wa Kizayuni.
Gazeti la Kizayuni la Jerusalem Post limemnukuu Evigdor Lieberman akitoa vitisho hivyo jana (Jumatatu) na kusema kuwa Wazayuni hawawezi kuvumilia jinsi makundi ya muqawama ya Palestina yanavyotumia vishada vya moto na kuendelea maandamano katika maeneo ya mpakani ya Ukanda wa Ghaza hivyo watalipiza kisasi kwa makundi ya Hamas, Jihadul Islami na mengineyo.
Waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni amedai kuwa, utawala huo hautaki kuubakisha katikati ugomvi wake na harakati za Hamas na Jihadul Islami.
Tangu tarehe 30 Machi mwaka huu hadi hivi sasa, wanajeshi makatili wa Israel wameshaua shahidi Wapalestina 130 katika maandamano ya amani yaliyoanza wakati wa maadhimisho ya mwaka wa 42 wa "Siku ya Ardhi" na maelefu ya Wapalestina wameshajeruhiwa.
Moja ya mbinu zinazotumiwa na harakati za mapambano ya Kiislamu za Palestina ni kutuma vishada vya moto katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na hadi sasa harakati hizo zimeusababishia hasara kubwa utawala katili wa Kizayuni kiasi kwamba waziri wa vita wa utawala huo ameshindwa kuvumilia na kutangaza bila kificho kuwa watamalizia hasira zao kwa harakati za Kiislamu za Hamas na Jihadul Islami.