Qatar yapinga hatua za Saudi Arabia huko Yemen
(last modified Fri, 22 Jun 2018 07:46:38 GMT )
Jun 22, 2018 07:46 UTC
  • Qatar yapinga hatua za Saudi Arabia huko Yemen

Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema kuwa nchi yake inapinga hatua za muungano vamizi wa Saudi Arabia huko Yemen.

Sheikh Muhammad bin Abdulrahman al Thani ambaye ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema akiwa katika Bunge la Ulaya kwamba njia pekee ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Yemen ni kufanyika mazungumzo na kuongeza kuwa, Doha inaunga mkono utulivu na usalama wa watu wa Yemen.   

Saudi Arabia ikiungwa mkono na Imarati, Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na baadhi ya waitifaki wake mwezi Machi mwaka 2015 iliivamia Yemen na kuizingira nchi kavu, baharini na angani nchi hiyo ya Kiarabu. Vita hivyo vya Saudia, Umoja wa Falme za Kiarabu na waitifaki wao huko Yemen hadi sasa vimeuwa raia wa Yemen zaidi ya elfu kumi, kuwajeruhi makumi ya maelfu na  kuwafanya mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.

Wakimbizi wa Yemen waliopata hifadhi makambini 
 

Hujuma hiyo ya jeshi la Saudia na Imarati pia imesababisha uhaba mkubwa wa chakula na dawa katika nchi hiyo maskini. Utawala wa Saudi Arabia na waitifaki wake hadi sasa umeshindwa kutimiza malengo yake huko Yemen ya kuwarejesha madarakani vibaraka wake kutokana na kusimama kidete watu wa Yemen. 

Tags