Saudia inahusika katika kuchelewesha uundaji wa serikali mpya ya Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i46785-saudia_inahusika_katika_kuchelewesha_uundaji_wa_serikali_mpya_ya_lebanon
Sheikh Nabil Qawooq mjumbe wa Baraza Kuu la harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameashiria uingiliaji kati wa Saudi Arabia katika suala la kuunda serikali huko Lebanon na kusisitiza kuwa viongozi wa Saudia ndio kikwazo kikuu na wanatatiza zaidi hali ya ndani ya Lebanon.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Jul 14, 2018 23:19 UTC
  • Saudia inahusika katika kuchelewesha uundaji wa serikali mpya ya Lebanon

Sheikh Nabil Qawooq mjumbe wa Baraza Kuu la harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameashiria uingiliaji kati wa Saudi Arabia katika suala la kuunda serikali huko Lebanon na kusisitiza kuwa viongozi wa Saudia ndio kikwazo kikuu na wanatatiza zaidi hali ya ndani ya Lebanon.

Baada ya ushindi wa harakati ya Hizbullah na waitifaki wake katika uchaguzi wa Bunge wa Mei 6 mwaka huu, Saudi Arabia na baadhi ya wanasiasa wa Lebanon wanafanya jitihada za kuunda mrengo wa wachache wenye nguvu ndani ya Bunge la nchi hiyo na kwa njia hiyo waweze kujipatia wizara nyingi katika baraza lijalo la mawaziri la serikali ya Lebanon.  Karibu miezi miwili sasa ambapo muhula wa Sa'ad Hariri wa kuunda serikali mpya nchini Lebanon unapita na hakujatolewa taarifa yoyote kuhusu kuchaguliwa na kuarifishwa bungeni majina ya mawaziri watarajiwa.

Wanamuqawama wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon 

Uchaguzi wa Bunge wa Lebanon ulifanyika katika mazingira ambayo  serikali za nchi ajinabi zikiongozwa na Saudi Arabia zilikuwa zikifanya njama kubwa kwa lengo la kuathiri matokeo ya uchaguzi huo. Hata hivyo licha ya mashinikizo hayo yote, wananchi wa Lebanon waliunga mkono kwa dhati kambi ya muqawama na kuchagua wawakilishi wake.  Licha ya ushindi huo mkubwa na wa kihistoria kambi ya muqawama kama ilivyokuwa umetangaza huko nyuma, umetangaza udharura wa kuwepo umoja wa kitaifa huko Lebanon na kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa nchini humo na wakati huo huo umemuunga mkono Waziri Mkuu, Sa'ad Hariri; kwa msingi huo Hariri alipewa mamlaka ya kuunda serikali kwa kupata kura 111.

Sa'ad Hariri, Waziri Mkuu wa Lebanon 

Kuhusu swali kwamba ni kwa nini hadi sasa Hariri ameshindwa kuunda serikali mpya nchini Lebanon, tunapasa kuzingatia mambo mawili au sababu za ndani na nje kuliko jambo lolote jingine. Katika uga wa ndani inaonekana kuwa pamoja na kuwa uchaguzi wa Bunge wa Lebanon umeweka wazi ushindi mkubwa wa kambi ya muqawama lakini baadhi ya pande zinafanya njama za kisiasa na kutaka mgao usio wa kimantiki katika serikali mpya ili kufidia hasara walizopata baada ya kupigwa mweleka na Hizbullah katika uchaguzi uliopita. 

Pamoja na kuweko vizuizi na vikwazo vyote hivyo, nchi ajinabi pia zimeazimia kukwamisha uundaji wa serikali mpya huko Lebanon kuliko wakati mwingine wowote. Katika mazingira haya mapya ambapo Saudi Arabia inahisi hatari kubwa kufuatia matokeo hayo ya uchaguzi wa wananchi wa Lebanon, inafanya juhudi za kukamishwa mchakato wa kuunda serikali mpya, na kupitia nia ya kupoteza wakati, imeazimia kuiweka madarakani serikali ambayo itakidhi matakwa yake. Saudi Arabia pamoja na Marekani zinafanya njama zote za kukwamisha mchakato wa kuunda serikali mpya nchini Lebanon.

Katika mazingira hayo Sa'ad Hariri ambaye amepewa jukumu la kuunda serikali mpya anaonekana kufanya uzembe na anaazimia kuunda serikali isiyooana na matokeo ya uchaguzi wa Bunge la Lebanon. Dosari ya Katiba ya Lebanon ya kutoainisha muda maalumu wa kuunda serikali baada ya uchaguzi wa Bunge ni miongoni mwa matatizo ya kisheria yanayotumiwa vibaya na Hariri kutimiza malngno yake na waitifaki wake kama Saudi Arabia. Hata hivyo iwapo makundi ya kisaisa ya Lebanon hususan wapinzani wa Hariri wataamua kuunda serikali nyingine wanaweza kumtaka Rais Michel Aoun amteue mtu mwingine kwa ajili ya kuunda serikali mpya ya Lebanon. Hata hivyo washirika katika mrengo wa Machi 8 unaoongozwa na Hizbullah hawataki kutumia wenzo huo kwa sasa ingawa ni chaguo lililoko mezani iwapo kutaendelea kuwepo ombwe wa kisaisa nchini Lebanon.