Silaha ya Muqawama; wenzo wa kuwahami wananchi wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i47410-silaha_ya_muqawama_wenzo_wa_kuwahami_wananchi_wa_palestina
Khalid al-Batsh, kiongozi mwandamizi wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amesisitiza kuwa silaha ya Muqawama ndio wenzo wa kulihami taifa na wananchi wa Palestina dhidi ya Wazayuni maghasibu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 13, 2018 03:00 UTC
  • Silaha ya Muqawama; wenzo wa kuwahami wananchi wa Palestina

Khalid al-Batsh, kiongozi mwandamizi wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amesisitiza kuwa silaha ya Muqawama ndio wenzo wa kulihami taifa na wananchi wa Palestina dhidi ya Wazayuni maghasibu.

Al-Batsh, ambaye ni afisa anayehusika na uhusiano wa nje katika harakati hiyo ya muqawama ya Palestina amefafanua kuwa silaha ya muqawama itayahami maandamano ya Haki ya Kurejea na kupeperusha bendera ya mapambano ya taifa la Wapalestina.

Khalid al-Batsh, Afisa wa uhusiano wa nje wa Jihadul-Islami

Katika kujibu uchokozi wa waziwazi wa ndege za kivita za utawala wa Kizayuni na mashambulio ya kinyama yaliyofanywa na ndege hizo katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza katika siku chache zilizopita, wanamapambano wa Muqawama wa Palestina nao pia wamejibu mapigo kwa kuvurumisha maroketi yasiyopungua 200 kuelekea ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, zilizopewa jina la Israel. "Jibu la moto ni moto", ndio mkakati ulioamuliwa kutekelezwa na makundi ya Muqawama wa Palestina ili kukabiliana na mashambulio ya kinyama ya Wazayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza. Ukweli ni kwamba ni vipigo vikali vya Muqawama ndivyo vilivyoufanya utawala wa Kizayuni ugonge mwamba na kushindwa kufikia malengo yake ya kibeberu na kujipanua katika ardhi za Palestina na hivyo kulazimika kurudi nyuma katika sehemu moja ya ardhi hizo, yaani Ukanda wa Gaza. Ahmad Bahr, Naibu Spika wa Bunge la Palestina ameizungumzia nukta hiyo kwa kusema: silaha ya muqawama ndiyo silaha pekee halali na ya kisheria ya kurejesha haki za Wapalestina na kuikomboa ardhi ya Palestina.

Makombora ya wanamuqawama wa Palestina yanayotumika kujihami na uchokozi wa wazayuni

Mapambano ya mtutu wa bunduki ya kukabiliana na wavamizi na maghasibu ni haki iliyokubalika na kutiliwa mkazo na sheria zote za kimataifa. Sisitizo la Wapalestina kwamba wataendeleza muqawama na kuendelea kubeba silaha ni jibu kwa njama na hila za utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake yakiwemo madola ya Magharibi hususan Marekani pamoja na baadhi ya tawala saliti za Kiarabu ambazo zinatumia mbinu mbalimbali kuwashawishi Wapalestina waachane na Muqawama na kuweka chini silaha. Dhamira ya utawala haramu wa Israel na waungaji mkono wake ni kudhoofisha na hatimaye kuufuta moja kwa moja Muqawama wa aina yoyote ile wa kukabiliana na sera za kujipanua za utawala huo katika ardhi za Palestina ili kwa njia hiyo uweze kufanikisha sera zake za kibeberu na kufikia malengo yake bila shida wala tabu yoyote.

Utawala wa Kizayuni unaibua maudhui mbalimbali ikiwemo ya kuwapokonya silaha Wapalestina ili utakapowadia wakati wa mazungumzo yoyote yale kuhusu kuundwa nchi ya Palestina uweze kuukubalisha mtazamo wake kwa Wapalestina wenyewe na kwa jamii ya kimataifa, ambao ni wa nchi ya aina hiyo kutokuwa na jeshi lolote. Ni katika mazingira haya ndipo tunashuhudia harakati mpya za utawala huo haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina zinazofanywa kwa baraka kamili za rais wa Marekani Donald Trump, ambaye naye pia ameibuka na mpango wenye hila na njama dhidi ya Wapalestina maarufu kwa jina la "Mapatano ya Karne", ambao moja ya malengo yake ni kuupokonya silaha Muqawama na kulizima moja kwa moja vuguvugu la Intifadha.

Katika kukabiliana na njama zote hizo, makundi ya Palestina yamesisitiza kwa mara nyengine kuwa kupokonywa silaha Muqawama ni moja ya mistari myekundu kwa Wapalestina, kwa sababu sheria na kanuni za kimataifa nazo pia zinalitambua suala la taifa kujilinda na kujihami kuwa ni halali kisheria.

Umma wa Wapalestina ukiunga mkono silaha ya Muqawama

Baada ya wananchi wa Palestina kujionea kwa macho yao ushindi na mafanikio uliyopata Muqawama katika miaka ya karibuni wa kutoa vipigo kadhaa kwa utawala wa Kizayuni katika uga wa kijeshi na kisiasa, sasa wananchi hao wamefikia hitimisho kuwa njia pakee ya kufikia malengo yao matukufu ni kuendeleza Muqawama na kusimama imara kukabiliana na utawala huo haramu.

Kuulazimisha utawala wa Kizayuni wa Israel urudi nyuma na kuondoka eneo la Ukanda wa Gaza mwaka 2005 na kuukwamisha utawala huo kufikia malengo yake katika vita vitatu ulivyoanzisha katika miaka ya karibuni dhidi ya eneo hilo kumeonyesha kuwa ni Muqawama pekee ndio ulioweza kuwapa Wapalestina matumaini ya kufikia malengo yao matukufu na kurejesha heshima na haki zao.../