Waingereza wapinga ushawishi wa lobi za Wazayuni katika siasa za London
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i47728-waingereza_wapinga_ushawishi_wa_lobi_za_wazayuni_katika_siasa_za_london
Zaidi ya Waingereza elfu kumi wamesaini waraka wakionesha upinzani wao dhidi ya lobi na makundi ya ushawishi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika siasa za nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 27, 2018 23:01 UTC
  • Waingereza wapinga ushawishi wa lobi za Wazayuni katika siasa za London

Zaidi ya Waingereza elfu kumi wamesaini waraka wakionesha upinzani wao dhidi ya lobi na makundi ya ushawishi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika siasa za nchi hiyo.

Waraka huo ambao hadi kufikia adhuhuri ya jana Jumatatu ulikuwa umesainiwa na zaidi ya Waingereza elfu kumi na 970 umesema kuwa Wazayuni wanafanya njama dhidi ya wanasiasa wa Uingereza wanaopinga jinai za utawala ghasibu wa Israel na wanawaondoa madarakani. 

Watu waliotia saini waraka huo wamesisitiza kuwa Waingereza hawakubali ushawishi wa nchi yoyote katika masuala yao ya kisiasa. Hii ni licha ya kwamba, Waziri Mkuu wa sasa wa Ungereza Thereza May amekataa wito wa kufanyika uchunguzi huru kuhusu satua na ushawishi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika siasa za Landon. 

Ripoti zinasema kuwa, serikali ya Uingereza inalazimika kujibu matakwa ya waraka uliosainiwa na raia zaidi ya elfu kumi.

Tangu miaka mitatu iliyopita yaani baada ya Jeremy Corbyn kuchaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha Leba nchini Uingereza, idadi kubwa ya wanachama wa chama hicho wamefutwa au kusimamisha kazi kwa muda kwa kisingizio cha eti kupinga Wayahudi.

Jeremy Corbyn ambaye ni miongoni mwa wabaharakati wa haki za binadamu, wapinzani wa vita na wapinzani wakubwa wa utawala ghasibu wa Israel amekuwa akilengwa sana kwa mashambulizi ya Wazayuuni nchini Uingereza. 

Jeremy Corbyn

Kabla ya kuchaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha Leba, Corbyn alikutana na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah na kusisitiza udharura wa kurejeshwa haki zilizoghusubiwa za Wapalestina. 

Ripoti zinasema kuwa makundi ya mashinikizo ya Wayahudi yanafanya harakati kubwa Ulaya na Marekani na yanawafutilia mbali wapinzani wao kwa kutumia kisingizio eti wanawapiga vita Wayahudi.