Imad Khamis: Hivi karibuni Syria itarejea katika hali yake ya kawaida
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i47954-imad_khamis_hivi_karibuni_syria_itarejea_katika_hali_yake_ya_kawaida
Waziri Mkuu wa Syria, Imad Khamis amesema kuwa kwa mara nyingine nchi hiyo itakuwa mchezaji muhimu katika nyuga tofauti kieneo na duniani na kwamba hivi karibuni taifa la Syria litarejea katika hali yake ya kawaida.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 07, 2018 03:16 UTC
  • Imad Khamis: Hivi karibuni Syria itarejea katika hali yake ya kawaida

Waziri Mkuu wa Syria, Imad Khamis amesema kuwa kwa mara nyingine nchi hiyo itakuwa mchezaji muhimu katika nyuga tofauti kieneo na duniani na kwamba hivi karibuni taifa la Syria litarejea katika hali yake ya kawaida.

Khamis ameyasema hayo katika ufunguzi wa Maonyesho ya 60 ya Kimataifa ya Damascus Ameongeza kuwa, azma ya Syria katika hatua mpya ni kuijenga upya nchi hiyo na kwamba, nchi yake imeweza kuushinda ugaidi na itafanikiwa katika kazi ya ujenzi mpya ikishirikiana na washirika wake. Amebainisha kwamba, nchi marafiki na ndugu wa Syria ambazo zilisimama pamoja na Damascus katika vita dhidi ya magaidi, zinayo fursa ya kuwekeza nchini humo.

Maonyesho ya 60 ya Kimataifa ya ya Damascus yalifunguliwa jana usiku na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Imad Khamis na yanayashirikisha mashirika 1700 ya ndani na nje kutoka nchi 48 za dunia.

Raia wa Syria wakishangilia ushindi mkubwa uliofikiwa dhidi ya magaidi

Katika maonyesho hayo Iran inawakilishwa na mashirika makubwa 52. Kufanyika maonyesho hayo kunatoa ujumbe wa kurejea usalama na amani nchini Syria na kuanza mwenendo wa ukarabati baada ya vita vya miaka kadhaa.

Mgogoro wa Syria uliibuka mwaka 2011 baada ya nchi za Saudi Arabia, Imarati, Marekani, utawala haramu wa Israel na washirika wao kuunda makundi ya kigaidi na kuyatuma nchini humo kwa ajili ya kuiondoa madarakani serikali halali ya Rais Bashar al-Assad na kuvuruga mlingano wa kijeshi na kisiasa katika eneo la Mashariki ya Kati kwa maslahi ya utawala khabithi wa Kizayuni.

Hivi karibuni jeshi la Syria likisaidiwa na washauri wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na uungaji mkono wa Russia, liliweza kufunga faili la kundi la kigaidi na kiwahabi la Daesh nchini humo.