Uturuki yazisaidia kifedha familia za wapinzani wa serikali ya Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i47973-uturuki_yazisaidia_kifedha_familia_za_wapinzani_wa_serikali_ya_syria
Duru za habari zimefichua uungaji mkono wa kifedha wa serikali ya Uturuki kwa familia za wapinzani wa serikali ya Syria waliouawa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 08, 2018 02:32 UTC
  • Uturuki yazisaidia kifedha familia za wapinzani wa serikali ya Syria

Duru za habari zimefichua uungaji mkono wa kifedha wa serikali ya Uturuki kwa familia za wapinzani wa serikali ya Syria waliouawa.

Kwa mujibu wa habari hiyo, serikali ya Ankara imeahidi kuzipatia misaada familia za wapiganaji wa upinzani waliouawa kutoka kundi la kigaidi linaloitwa 'Jeshi Huru la Syria' ambapo mbali na uungaji mkono wa kifedha, itazipatia makazi na nyenzo muhimu za kimaisha nchini humo. Vyombo vya habari vimemnukuu mmoja wa wanachama wa kundi hilo anayejulikana kwa jina la Abdullah Halawa akisema kuwa, serikali ya Uturuki imezipatia familia za wapiganaji wa genge hilo kiasi cha Dola elfu tisa.

Nembo ya kundi la kigaidi la Jeshi Huru linalopewa msaada wa kifedha na Uturuki.

Halawa ameongeza kwamba, serikali ya Uturuki pia inaendelea kuwasaidia kifedha majeruhi wa kundi hilo maarufu kwa kutenda jinai dhidi ya binaadamu. Inafaa kuashiria kuwa, jeshi la Uturuki kwa kushirikiana na wapiganaji wa kundi la Jeshi Huru la Syria, lilianzisha mashambulizi makali dhidi ya mji wa Afrin, kaskazini mwa Syria Januari mwaka huu. Hii ni katika hali ambayo kwa mara kadhaa serikali ya Damascus imeitaja operesheni ya kijeshi ya Uturuki katika ardhi yake kuwa ni uvamizi na ukiukaji wa haki ya kujitawala sambamba na kulaani hatua hiyo.