Mufti wa Syria: Ushindi wa nchi yetu ni ushindi wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i48618-mufti_wa_syria_ushindi_wa_nchi_yetu_ni_ushindi_wa_palestina
Mufti Mkuu wa Syria, Sheikh Ahmad Badreddin Hassoun amesema kuwa ushindi wa Syria dhidi ya ugaidi ni ushindi wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 06, 2018 11:43 UTC
  • Mufti wa Syria: Ushindi wa nchi yetu ni ushindi wa Palestina

Mufti Mkuu wa Syria, Sheikh Ahmad Badreddin Hassoun amesema kuwa ushindi wa Syria dhidi ya ugaidi ni ushindi wa Palestina.

Sheikh Hassoun amesema hayo katika mji wa Quneitra ulioko kwenye milima ya Golan na kuongeza kuwa, maadui wa Syria ndio hao hao maadui wa Palestina ambao wanafanya njama dhidi ya mji mtakatifu wa Quds na ardhi nyingine za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Mufti Mkuu wa Syria ametilia mkazo wajibu wa kuendelezwa mapambano dhidi ya ugaidi hadi Syria itakaposafishwa kikamilifu na uwepo wa magaidi hao wakufurishaji.

Mwanajeshi wa Syria akipeperusha bendera juu ya nchi yake baada ya kufurushwa magaidi katika mji wa Quneitra

 

Milima ya Golan ni eneo lililoko kusini magharibi mwa Syria ambapo mwaka 1967 utawala wa Kizayuni wa Israel uliteka sehemu moja ya eneo hilo na kulikalia kwa mabavu hadi hivi sasa.

Mgogoro wa Syria ulianzishwa mwaka 2011 kwa kuvamiwa na magenge mengi ya magaidi kutoka kila kona ya dunia kwa msaada wa Saudia, Marekani, Israel na waitifaki wao. Lengo la magaidi hao ni kuivuruga Syria ili kulinda usalama wa utawala wa Kizayuni. Hata hivyo kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu, juhudi za jeshi na wananchi wa Syria zimefanikiwa kuzima njama hiyo kubwa ya maadui.