Kumbukumbu ya kuuawa shahidi Sheikh Nimr Baqir Al Nimr + Filamu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i50581-kumbukumbu_ya_kuuawa_shahidi_sheikh_nimr_baqir_al_nimr_filamu
Leo Jumatano Januari Pili 2019 ni kumbukumbu ya mwaka wa tatu tokea alipouawa shahidi Sheikh Nimr Baqri al Nimr, mwanazuoni wa Kiislamu na mwanamapambano wa kutetea haki wa Saudi Arabia
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Jan 02, 2019 04:21 UTC
  • Kumbukumbu ya kuuawa shahidi Sheikh Nimr Baqir Al Nimr + Filamu

Leo Jumatano Januari Pili 2019 ni kumbukumbu ya mwaka wa tatu tokea alipouawa shahidi Sheikh Nimr Baqri al Nimr, mwanazuoni wa Kiislamu na mwanamapambano wa kutetea haki wa Saudi Arabia

Sheikh Nimr Bari al Nimr, mwanazuoni maarufu wa Saudia alikamatwa na utawala wa ukoo wa Aal Saudi manamo Julai 2012 na hatimaye Oktoba 2015, mahakama ya utawala wa Saudia ilimhukumu msomi huyo wa Kiislamu kifo cha kukatwa kichwa kwa panga na kusulubiwa kadamnasi kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kula njama dhidi ya utawala wa nchi hiyo..

Hukumu hiyo ilitekelezwa tarehe Pili Januari mwaka 2016. Kuuawa kwa msomi na mwanaharakati huyo kulipingwa vikali na jumuiya za kikanda na kimataifa za kutetea haki za binadamu.   

Mwanazuoni huyo wa Kiislamu daima alikuwa akikosoa siasa za ukandamizaji na za kibaguzi za utawala wa kifalme wa Saudia na alifungwa jela mara kadhaa kutokana na kusema haki na kweli.