Lebanon yamtia nguvuni jasusi wa utawala haramu wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i51063-lebanon_yamtia_nguvuni_jasusi_wa_utawala_haramu_wa_israel
Jeshi la Lebanon limemtia mbaroni ajenti wa Shirika la Ujasusi la Utawala wa Kizayuni wa Israel (Mossad) aliyehusika katika shambulizi la bomu kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 23, 2019 04:23 UTC
  • Lebanon yamtia nguvuni jasusi wa utawala haramu wa Israel

Jeshi la Lebanon limemtia mbaroni ajenti wa Shirika la Ujasusi la Utawala wa Kizayuni wa Israel (Mossad) aliyehusika katika shambulizi la bomu kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu.

Idara ya Intelijensia ya Jeshi la Lebanon imeripoti kuwa, wakala huyo wa Mossad alikamatwa juzi (Januari 21) katika eneo la Sharhabeel, katika mji wa Sidon, yapata kilomita 40 kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut.

Taarifa ya idara hiyo imemtaja ajenti huyo wa Israel kuwa ni Hussein Ahmad Batto, ambaye anadaiwa kuhusika katika shambulizi la bomu la kutegwa garini lililomjeruhi ofisa wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) mwaka jana.

Nembo ya Mossad na washirika wake

Ajenti huyo wa utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kwamba amekuwa akiifanyia kazi Mossad tangu mwaka 2014, na kuwa yeye pamoja na majasusi wawili wa Israel walihusika katika mauaji ya kigaidi ya Mohammed Hamdan Januari 14 mwaka jana.  

Julai mwaka jana gazeti la Daily Mail la Uingereza liliripoti kuwa, Shirika la Ujasusi la Israel Mossad linaongoza duniani kwa kufanya mauaji ya kigaidi na kwamba katika kipindi cha miaka 10 tu iliyopita Mossad imefanya operesheni 800 za mauaji ya kigaidi ambazo zimepelekea kuuawa maelfu ya watu.