Wizara ya Elimu Palestina yaonya kuhusu kubadilishwa muundo wa masomo
Wizara ya Elimu ya Juu ya Palestina imeonya kuhusiana na njama yoyote ile inayolenga kubadilishwa muhtawa wa masomo wa Wapalestina.
Taarifa ya Wizara ya Elimu ya Juu ya Palestina imeashiria misaada ya kifedha iliyotolewa kwa taasisi za kielimu za utawala haramu wa Israel ili zikabiliane na mfumo wa elimu wa Palestina pamoja na muhatawa wake na kutangaza kuwa, taasisi za kielimu za Israel zimekuwa zikitoa tuhuma zisizo na maana kama vile eti mfumo wa elimu wa Wapalestina umejaa uchochezi zikifanya njama za kutaka kubadilishwa muundo huo wa kielimu.
Wizara ya Elimu ya Juu ya Palestina imeeleza kwamba, miaka miwili iliyopita, wizara hiyo iliitaka tume moja huru ilinganishe baina ya mfumo wa kielimu wa Palestina na wa utawala haramu wa Israel na matokeo yake kinyume kabisa na madai ya Israel, mfumo wa elimu wa Palestina ukaonekana kuwa unalenga kuwafundisha wanachuo thamani aali kama umuhimu wa kujifunza elimu na kuondoa ujinga.
Itakumbwa kuwa, kumekuwa kukishuhudiwa njama mbalimbali za Israel za kama kuondoa nara za muqawama katika majalada ya vitabu vya kufundishia mashuleni, kufuta bendera ya Palestina na nembo nyingine zinazohusiana na mapambano ya kitaifa lengo likiwa ni kuubadilisha mfumo wa elimu wa Palestina na kuufanya kuwa wa Kiyahudi.