UN: Wapalestina 1,700 wa Gaza katika hatari ya kukatwa miguu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i53373-un_wapalestina_1_700_wa_gaza_katika_hatari_ya_kukatwa_miguu
Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imeeleza wasiwasi mkubwa ilionao kutokana na kuzidi kuwa mbaya hali ya kibinadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, na kubainisha kuwa mamia ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wako katika hatari ya kusababishiwa ulemavu wa maisha kutokana na majeraha ya risasi za jeshi katili la utawala wa Kizayuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 09, 2019 08:03 UTC
  • UN: Wapalestina 1,700 wa Gaza katika hatari ya kukatwa miguu

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imeeleza wasiwasi mkubwa ilionao kutokana na kuzidi kuwa mbaya hali ya kibinadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, na kubainisha kuwa mamia ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wako katika hatari ya kusababishiwa ulemavu wa maisha kutokana na majeraha ya risasi za jeshi katili la utawala wa Kizayuni.

Mratibu wa OCHA katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, Jamie McGoldrick amesema kukauka mfuko wa afya huenda kukapelekea Wapalestina 1,700 wakakatwa miguu katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Afisa huyo wa UN amesema umoja huo unahitaji msaada wa dola milioni 20 kwa ajili ya kutoa huduma za kimsingi za afya kwa Wapalestina hao wa Ukanda wa Gaza ambao ardhi zao zinakaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Kwa mujibu wa Mratibu huyo wa Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA), Wapalestina 29 elfu wamejeruhiwa katika maandamano huko Ukanda wa Gaza, ambapo 7,000 miongoni mwao wanauguza majeraha ya risasi.

Maandamano ya Haki ya Kurejea

Amebainisha kuwa, 1,700 miongoni mwao wanahitaji kufanyiwa upasuaji wa dharura wa miguu ili waweze kutembea tena.    

Amesema Wapalestina 120 wakiwemo watoto 20 wamekatwa miguu kutokana na majeraha mabaya ya risasi za wanajeshi wa Israel ndani ya mwaka mmoja uliopita. 

Maandamano ya "Haki ya Kurejea" yalianza rasmi tarehe 30 Machi mwaka jana 2018 na yamekuwa yakifanyika kila Ijumaa, ambapo hadi sasa mamia ya Wapalestina wameshauliwa shahidi na wengine wanaokaribia 30 elfu wamejeruhiwa.