Vikao vya Makka; uchochezi ambao unaweka wazi kuchanganyikiwa Saudi Arabia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i53843-vikao_vya_makka_uchochezi_ambao_unaweka_wazi_kuchanganyikiwa_saudi_arabia
Katika siku za Alhamisi na Ijumaa, Saudi Arabia iliandaa vikao vitatu katika mji mtakatifu wa Makka. Vikao hivyo vilikuwa vya kuhudumia ajinabi na maadui wa umma wa Kiislamu na wakati huo huo vimebainisha wazi kuchanganikiwa na kupoteza mwelekeo watawala wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 01, 2019 07:26 UTC
  • Vikao vya Makka; uchochezi ambao unaweka wazi kuchanganyikiwa Saudi Arabia

Katika siku za Alhamisi na Ijumaa, Saudi Arabia iliandaa vikao vitatu katika mji mtakatifu wa Makka. Vikao hivyo vilikuwa vya kuhudumia ajinabi na maadui wa umma wa Kiislamu na wakati huo huo vimebainisha wazi kuchanganikiwa na kupoteza mwelekeo watawala wa nchi hiyo.

Siku ya Alhamisi, Saudi Arabia iliitisha kikao cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na pia kikao cha Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi katika mji wa Makka na siku ya Ijumaa pia mji huo ulikuwa mwenyeji wa kikao cha nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC.

Nukta ya kutaamali katika kufanyika vikao hivyo ni kuwa vimefanyika sambamba na Siku ya Kimataifa ya Quds. Katika vikao hivyo mjini Makka na kabla ya hapo pia katika vikao vya Manama na Jeddah, wakuu wa Saudia walikuwa wanalenga  kuisahaulisha au kuihafifisha Siku ya Kimataifa ya Quds na kuibua mifarakano kuhusu siku hiyo.

Swali linaloibuka ni hili kuwa, je, lengo la hadaa hizo zote ni nini hasa?

Tukiangazia matukio ya huko nyuma tunaweza kupata jibu la swali hili muhimu. Cheche ya kwanza ya mpango wa kuwafanya Wapalestina na Waarabu wawe na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel ilikuwa mwaka 1993 katika kongamano la  "Oslo". Hata habla ya kuwepo ishara za amani au kufikiwa haki za kimsingi za taifa la Palestina, faili la kongamano hilo lilifungwa. Miaka 14 baadaye, Rais George W Bush wa Marekani alitoa pendelezo la kongamano la amani na 'Annapolis' na hapo pia hapakujiri chochte zaidi ya kilichojiri 'Oslo'.  Baada ya hapo pia kulijiri vikao kadhaa kuhusu Palestina kama kile cha 'Amani ya Majira ya Vuli' lakini vyote vilifeli. Sababu ya kufeli vikao hivyo ni kuwa vyote vilikuwa na nukta moja ya pamoja nayo ni kuunga mkono wazi wazi utawala wa Kizayuni wa Israel kwa madhara ya Palestina. Leo pia nyayo za vikao hivyo vilivyofeli zinaonekana wazi katika vikao ambavyo vimefanyika Alhamisi na Ijumaa mjini Makka.

Waziri Mkuu wa utawala za Kizayuni Yitzhak Rabin, Rais wa Marekani Bill Clinton, na kiongozi wa PLO Yasser Arafat katika sherehe za utiwaji saini mapatano ya Oslo  13 Septemba 1993

Uzoefu wa miaka yote hiyo umeonyesha kuwa kuanzia  'Kongamano la Oslo' hadi mpango wa 'Muamala wa Karne' hakuna chochote kinachofuatiliwa ambacho kinaweza kuleta amani na utulivu endelevu katika eneo la Asia Magharibi au Mashariki ya Kati. Hii ni kwa sababu haki za taifa madhulumu la Palestina zinaweza kudhaminiwa tu kwa kurejea nyumbani wakimbizi wote wa Palestina na kufanyika kura ya maoni itakayowashirikisha wakaazi wote wa asili wa ardhi hiyo ili wainishe hatima yao.

Historia inaonyesha kuwa, uwepo wa utawala wa Kizayuni wa Israel umejengeka katika msingi wa mauaji ya kigaidi, kukalia kwa mabavu ardhi za wengine, vita na vitisho. Utawala unaotenda jinai wa Israel umetekeleza aina kadhaa za mauaji ya umati na kimbari na jinai dhidi ya binadamu katika kipindi cha miongo sabini cha kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

Leo lengo la utawala wa Kizayuni ni kuimarisha mizizi ya ukaliaji mabavu ardhi za Palestina kwa kuibua migogoro katika eneo na kuunda miungano yenye kuibua mifarakano na ni kwa msingi huo ndio tunaona leo utawala wa Saudia unashirikiana na utawala wa Israel katika kuibua migogoro.

Mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel

Hassan Hanizadeh, mchambuzi wa masuala ya Asia Magharibi katika mazungumzo na jarida la Quds Online anaashiria nukta hii ambapo amechambua vikao vya Makka ifuatavyo:

"Kutokana na kufeli kijeshi Saudi Arabia nchini Yemen na pia kufeli sera zake katika eneo, hivi sasa wakuu wa Saudia wanajaribu kuzishawishi Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kuwa na msomamo wa pamoja dhidi ya Iran. Huko nyuma pia Saudia ilijaribu kuunda muungano wa Kiibrania-Kiarabu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lakini ikafeli na kulipa gharama kubwa ya kisiasa.

Kama alivyosema Sayyed Abbas Musavi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran,  katika radiamali yake kuhusu Saudia kutumia vibaya uwenyeji wake wa vikao hivyo kwa ajili ya kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Iran; Jitihada za Saudi Arabia na baadhi ya nchi za Kiarabu katika eneo zenye lengo la kusambararatisha malengo ya ukombozi wa Palestina na mahala pake kuainisha malengo bandia na yasiyo na maana ni kosa la kistratijia.

Hakuna shaka kuwa, propaganda za Saudia dhidi ya Iran katika vikao vya Makka ni njama inayotekelezwa kwa lengo la kuuweka ulimwengu wa Kiislamu mbali na kadhia ya Palestina ambayo ni kadhia muhimu zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu, lakini vikao hivyo havina natija nyingine ila kuweka wazi namna Saudia ilivyochanganyikiwa.