Radiamali ya EuroMed Rights kufuatia kubomolewa nyumba za Wapalestina
(last modified Sun, 11 Aug 2019 04:10:58 GMT )
Aug 11, 2019 04:10 UTC
  • Radiamali ya EuroMed Rights kufuatia kubomolewa nyumba za Wapalestina

Shirika la kutetea haki za binadamu la EuroMed Rights limekitaja kitendo cha utawala wa Kizayuni cha kubomoa nyumba za Wapalestina kuwa ni maangamizi ya kizazi.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limetoa taarifa na kueleza kuwa jinai za Israel dhidi ya raia wa Palestina huko Quds ambazo zinatekelezwa kwa malengo maalumu zinafanyika kwa uungaji mkono wa serikali ya Marekani huku taasisi na duru za kimataifa zikinyamaza kimya bila ya kuchukua hatua yoyote. 

Ripoti ya shirika hilo la EuroMed Rights inaeleza kuwa, kuanzia mwaka 1967 hadi mwezi Julai mwaka huu wa 2019 Israel imetekeleza oparesheni kubwa zaidi ya ubomoaji nyumba za Wapalestina katika siku moja tu. 

Moja ya nyumba za Wapalestina zilizobomolewa na Israel katika mji wa Quds
 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, majengo 11 ambayo yalikuwa na jumla ya nyumba 72 za makazi za raia wa Palestina yamebomolewa katika siku moja pekee.  Shirika la haki za binadamu la EuroMed Rights limezitolea wito taasisi za kimataifa zitekeleza majukumu yao kuhusu mji wa Quds na raia wa Palestina kwa mujibu wa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Baraza Kuu la umoja huo kwa kuzingatia kuwa raia hao ni wakazi wa eneo linalokaliwa kwa mabavu. Utawala wa Kizayuni unaendelea kubomoa nyumba za Wapalestina na kujenga za walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya wananchi hao waliodhulumika kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa.  

Tags