Magaidi walioua watu katika maandamano ya Iraq watiwa nguvuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i56970-magaidi_walioua_watu_katika_maandamano_ya_iraq_watiwa_nguvuni
Kamanda wa Operesheni ya Baghdad amesema kuwa magaidi waliowalenga na kuua raia wanaoandamana nchini humo wametiwa nguvuni.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 31, 2019 10:34 UTC
  • Magaidi walioua watu katika maandamano ya Iraq watiwa nguvuni

Kamanda wa Operesheni ya Baghdad amesema kuwa magaidi waliowalenga na kuua raia wanaoandamana nchini humo wametiwa nguvuni.

Meja Jenerali Qays al-Muhammadawi  amesema kuwa, magaidi wanaowapiga risasi na kuwaua waandamanaji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Baghdad wamekamatwa na vyombo husika. 

Al Muhammadawi pia amewataka raia wa Iraq kuheshimu sheria ya marufuku ya kutembea iliyowekwa katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad.

Baadhi ya miji ya Iraq imekumbwa na maandamano ya wananchi wanaolalamikia ushuru uliowekwa na serikali na mgogoro wa kiuchumi unaoisumbua nchi hiyo. Pamoja na hayo kuna ushahidi unaoonesha kuwa, maandamano hayo yanachochewa zaidi na madola ya kigeni kwa kutumia vibaraka wao wa ndani. 

Maandamano ya Wairaqi, Baghdad

Wakati huohuo ripoti zinaeleza kuwa asilimia 79 ya jumbe ambazo zimetumwa katika mtandao wa kijamii wa Twitter kuhusu maandamano ya Iraq zinatoka kwa watumiaji wa mtandao huko walioko nchini Saudi Arabia.