Hamas yatungua 'drone' ya jeshi la Israel Ukanda wa Gaza
(last modified Tue, 28 Apr 2020 07:14:20 GMT )
Apr 28, 2020 07:14 UTC
  • Hamas yatungua 'drone' ya jeshi la Israel Ukanda wa Gaza

Harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) imefanikiwa kutungua ndege isiyo na rubani ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti kuwa, 'drone' hiyo ya Wazayuni imetungulia na vikosi vya Hamas mashariki mwa jiji la Dir al-Balah, katika Ukanda wa Gaza na hivi sasa ipo mikononi mwa wanamuqawama hao.

Jeshi la utawala haramu wa Israel linadai kuwa ndege yake hiyo isiyo na rubani imedondoka kutokana na hitilafu za kifundi, na eti ni muhali kuvujisha taarifa zozote muhimu kutoka kwenye chombo hicho.

Drone za utawala haramu wa Israel hutunguliwa mara kwa mara Palestina, Lebanon na Syria

Vikosi vya muqawama vya Palestina mara kwa mara vimekuwa vikitungua 'drone' za utawala pandikizi wa Israel, ambazo hutumiwa na utawala huo wa Kizayuni katika operesheni za mauaji na ujasusi.

Mbali na Palestina, ndege hizo zisizo na rubani za utawala haramu wa Israel zimekuwa zikiruka kinyume cha sheria katika anga za Syria na Lebanon. Utawala ghasibu wa Israel umekuwa ukitumia drone katika hujuma na mapambano ya kukabiliana na harakati za muqawama wa Kiislamu.

Tags