Hamas yalaani hatua ya Wazayuni ya kubomoa vituo vya Wapalestina
(last modified Thu, 18 Jun 2020 02:52:55 GMT )
Jun 18, 2020 02:52 UTC
  • Hamas yalaani hatua ya Wazayuni ya kubomoa vituo vya Wapalestina

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kuwa kitendo cha utawala wa Kizayuni wa Israel cha kubomoa vituo vya Wapalestina huko Quds inayokaliwa kwa mabavu ni jitihada za utawala huo zinazolenga kubadili utambulisho wa Quds; njama ambazo hazitafikia popote.

Msemaji wa harakati ya Hamas, Hazim Qassim amesema kuwa kitendo cha utawala wa Kizayuni cha kubomoa vituo vya Wapalestina huko Quds kinadhihirisha ukiukaji wa sheria za kimataifa na kushambuliwa raia wa Palestina kunakoendelea kufanywa na Israel. Amesema, sheria za kimataifa zinatambua hatua hiyo ya Wazayuni kuwa ni jinai ya kivita. 

Msemaji wa Hamas ameongeza kuwa vita vya Wazayuni vya kutaka kuharibu utambulisho wa mji wa Quds vitafeli na kushindwa mbele ya istiqama, irada na kusimama imara kwa wananchi wa Palestina ambao wako tayari kusabilia roho zao kwa ajili ya kuilinda Quds na utambulisho wa Palestina. 

Hazim Qassim amesema kuwa, harakati za utawala wa Kizayuni za kutaka kuiyahudisha Quds na kuuvunjia heshima Msikiti wa al Aqsa sambamba na njama zinazofanywa na pande kadhaa katika eneo hili za kuhusisha uhusiano wao na maghasibu wa Kizayuni, vimeongezeka. 

Msikiti wa al Aqsa kibla cha kwanza cha Waislamu  

 

Tags