Bahrain yasema itawafunga jela wanaopinga uhusiano wake na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i64011-bahrain_yasema_itawafunga_jela_wanaopinga_uhusiano_wake_na_israel
Utawala wa kifalme Bahrain umesema utawakamata na kuwafunga jela wale wote wanaopinga uhusiano wa nchi hiyo na utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 14, 2020 08:01 UTC
  • Bahrain yasema itawafunga jela wanaopinga uhusiano wake na Israel

Utawala wa kifalme Bahrain umesema utawakamata na kuwafunga jela wale wote wanaopinga uhusiano wa nchi hiyo na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika taarifa, Waizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain imesema wale ambao wanatumia mitandao ya kijamii kupinga mapatano na Israel watakabiliwa na shtaka la kuichafulia jina nchi hiyo.

Wizara hiyo imedai kampeni ya mitandao ya kijamii ya kupinga uhusiano na Israel inavuruga amani na uthabiti.

Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain baada ya kufikia mapatano na utawala wa Kizayuni wa Israel unaoikalia Quds kwa mabavu; tarehe 15 mwezi Septemba mwaka huu zilisaini huko White mapatano ya kuanzisha uhusiano rasmi na utawala huo wa Kizayuni.

Wapinzani Bahrain wakiwa na picha ya mfalme wa nchi hiyo Hamad bin Isa bin Salman Al Khalifa 

Tukio hilo lilihudhuriwa na Rais Donald Trump wa Marekani na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Waislamu na wapenda haki kote duniani wamekitaja kitendo hicho cha UAE na Bahrain kama usaliti na ni sawa na kuwachoma jambia kwa nyuma wananchi madhulumu wa Palestina.