HAMAS: Njia pekee ya kukabiliana na uvamizi ni muqawama
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i64069-hamas_njia_pekee_ya_kukabiliana_na_uvamizi_ni_muqawama
Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS sambamba na kukataa takwa la Marekani la kufanya mazungumzo amesema kuwa, njia pejkee ya kukabiliana na uvamizi nai muqawama na mapambano.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 17, 2020 04:20 UTC
  • HAMAS: Njia pekee ya kukabiliana na uvamizi ni muqawama

Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS sambamba na kukataa takwa la Marekani la kufanya mazungumzo amesema kuwa, njia pejkee ya kukabiliana na uvamizi nai muqawama na mapambano.

Saleh al-Arouri amesema hayo leo na kusisitiza kwamba, Hamas imekataa kufanya mazungumzo na Marekani kuhusiana na mpango uliojaa njama wa Muamala wa Karne ambao kimsingi unapora na kukanyaga haki za Wapalestina.

Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameongeza kuwa, harakati hiyo imekataa ombi hilo kwani inaonekana Marekani kupitia mpango huu inafanya njama za kuzusha hitilafu baina ya makundi ya Kipalestina.

Aidha Saleh al-Arouri amebainisha kuwa, njia ya kisiasa ambayo msingi wake ni mazungumzo kwa usimamizi wa Marekani ilifikia katika mkwamo na kila mafanikio yaliyopatikana kuhusiana na kadhia ya Palestina ni kwa baraka za muqawama na kusimamam kidete.

Saleh al-Arouri, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS

 

Kuhusiana na uchaguzi wa Palestina, afisa huyo wa Hamas amesema, harakati yao na ile ya Fat;hi zikiwa na umoja na ushiriki wa kitaifa zitashiriki katika uchaguzi na kuanzisha vita vimoja vya kukabiliana na mipango michafu ya utawala haramu wa Israel.

Kiongozi huyo mwandamizi wa Hamas ameashiriia hatua ya baadhi ya mataifa ya Kiarabu ya kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel na kusisitiza kwamba, mataifa ya Imarati na Bahrainb kwa hatua yao hiyo wameanzisha moja ya nji za kuitokomeza kadhia ya Palestina.